Shinyanga
Mkuu wa Wilaya ya
Shinyanga Mhe. Johari Samizi ameitaka jamii, viongozi wa serikali pamoja na
wadau mbalimbali kushirikiana ili kutokomeza mmomonyoko wa maadili kama ukatili, mapenzi na ndoa za jinsia moja.
Ameyasema hayo leo wakati
akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM ya
Mwaka 2022/2023 kipindi cha Julai hadi Disemba Mwaka 2022 kwenye mkutano ambao
umefayika katika ukumbi wa ofisi za CCM Wilaya ya Shinyanga mjini.
DC Samizi amesema ushirikiano wa kupambana dhidi ya
mmomomnyoko wa maadili utasaidia kuendelea kukuza na kulinda mila, desturi na
maadili mema ya Kitanzania.
Katika hatua nyingine mkuu
huyo wa wilaya amesema serikali itaendelea kufanya jitihada
mbalimbali kuhakikisha inachukua hatua kali kwa taasisi zitakazo bainika
kujihusisha na uhamasishaji mapenzi na ndoa za jinsia moja katika Wilaya ya
Shinyanga.
Kwa upande wake
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga mjini Bwana Anord Makombe amesema
serikali iendelee kuchukua hatua kali kwa wanaobainika kufanya mambo hayo
katika jamii.
Naye katibu wa CCM wa
Wilaya hiyo Bwana Ally Ally amewasihi wananchi kuungana na serikali kupinga
vitendo hivyo ili kuimarisha usalama wa Taifa.
Wakati huo huo leo Wajumbe
wa Halmashauri kuu ya CCM Wilaya ya Shinyanga mjini wamepokea taarifa ya
utekelezaji wa ilani ya chama hicho ya Mwaka 2022/2023 katika kipindi cha Julai
hadi Disemba Mwaka 2022.