Hukumu ya jamal malinzi na wenzake watatu kutolewa mwezi ujao



Hatima
ya Rais wa zamani wa Shirikisho la Soka (TFF), Jamal Malinzi na wenzake
watatu kurudi uraiani au la itajulikana Novemba 7,mwaka huu
watakaposomewa hukumu.


Malinzi
na wenzake wanakabiliwa na mashtaka 20 yakiwamo ya kula njama,
kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji wa
fedha wa USD 173,335.

Uamuzi
huo ulisomwa jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaidi, baada ya
Hakimu Mkazi Maira Kasonde aliyesikiliza kesi hiyo kuwa na udhuru.

Hakimu alisema baada ya kusikiliza ushahidi wa mashahidi wa pande zote mbili, mahakama yake itatoa hukumu mwezi ujao.

Wakili
wa Serikali Ester Martin alidai kuwa kesi hiyo ilipangwa kwa ajili ya
kupanga tarehe ya hukumu na kwamba upande wa Jamhuri uko tayari.

Hakimu Shaidi alisema kesi hiyo itasomwa hukumu tarehe iliyopangwa na kuamuru washtakiwa warudishwe mahabusu.