Igp sirro aagizwa kupeleka timu ya wataalamu ujenzi kituo cha polisi ikungi

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(katikati) na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi
wakikagua Ujenzi wa Makao  wakitoka kukagua Mradi wa Makao Makuu ya
Polisi wilayani hapo, leo ikiwa ni harakati za kujenga kituo kipya
wilayani hapo.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward
Mpogolo, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni
na Mbunge wa Singida Mashariki, Miraji Mtaturu pamoja na viongozi
wengine wilayani Ikungi, wakitoka kukagua Mradi wa Makao Makuu ya Polis
wilayani hapo(pichani), leo ikiwa ni harakati za kujenga kituo kipya
wilayani hapo.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Mbunge wa Singida Mashariki,
Miraji Mtaturu (kulia), Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi
Hamad Masauni(katikati) na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi,Edward Mpogolo
wakiongozana kuingia katika kituo chakavu cha polisi , leo wilayani
Ikungi mkoani Singida. Serikali iko mbioni kujenga kituo kipya ikiwa ni
moja kati ya hatua ya kuhamisha kituo hicho pichani ambacho ni chakavu.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Mbunge wa Singida Mashariki,
Miraji Mtaturu,akimuongoza  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mhandisi Hamad Masauni(watatu)kutoka nje ya  Kituo cha Polisi Ikungi ,
leo wilayani Ikungi mkoani Singida. Serikali iko mbioni kujenga kituo
kipya ikiwa ni moja kati ya hatua ya kuhamisha kituo hicho pichani
ambacho ni chakavu.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Na Mwandishi Wetu
Naibu Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad amemuagiza Mkuu wa Jeshi la
Polisi nchini, IGP Simon Sirro kutuma timu ya wataalamu kutoka Makao
Makuu ya Jeshi la Polisi kufika wilayani Ikungi Mkoani Singida,
kutathmini maendeleo ya Ujenzi wa Ofisi na Kituo kipya cha Polisi baada
ya kituo cha awali kuchakaa hali inayopelekea askari na mahabusu kukaa
sehemu isiyo salama.
Ameyasema hayo
leo wakati wa ziara ya kutembelea Wilayani Ikungi ikiwa ni kuitikia wito
wa Mbunge wa Singida Mashariki, Miraji Mtaturu, aliyetaka kauli ya
Serikali juu ya uchakavu wa Ofisi, kituo cha polisi Ikungi na hali mbaya
ya chumba cha mahabusu wakati wa kipindi cha maswali katika kikao cha
Bunge kilichoisha hivi karibuni.
“Nimefika hapa
nimeona mazingira wanayofanyia kazi hayaridhishi, serikali ilishaanza
Ujenzi wa Ofisi ya Makao Makuu ya Polisi ya Wilaya lakini ujenzi
umesimama kwa miaka mitano sasa, namuagiza IGP Sirro alete wataalamu
waje wafanye tathmini juu ya gharama za umalizwaji ujenzi huu na baada
ya kujua basi hatua za haraka zifanyike ili ujenzi huu ukamilike”
alisema Masauni
Akizungumza
wakati wa ziara hiyo, Mbunge wa Singida Mashariki, Miraji Mtaturu
amesema hali ya kituo cha polisi hicho ni mbaya huku mahabusu wakikaa
sehemu chafu ambayo si salama kwa afya ya binadamu.
“Mheshimiwa
Naibu Waziri kama nilivyokueleza bungeni wakati nikiuliza swali la
nyongeza nadhani sasa umejionea hali ilivyo mbaya, humo ndani umesikia
harufu katika chumba cha mahabusu,wanajisaidia humo lakini pia umeona
askari wanavyofanya kazi kwenye mazingira mabovu, naomba sasa serikali
muangalie uwezekano wa kuharakisha kituo kile kipya hata mkianza na
sehemu tu itasaidia adha hii wanayopata wananchi wa wilaya hii” alisema
Mbunge Mtaturu.
Nae Mkuu wa
Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogoro amesema uwepo wa kituo hicho kipya
kikikamilika kitaimarisha Ulinzi na Usalama wilayani hapo ambapo kumekua
na changamoto za kiusalama kwasababu ya upya wa wilaya hiyo ambayo
imeanza.