Igp sirro awaonya vikali askari polisi,ahaidi kuwafukuza kazi wanao kwenda kinyume na jeshi hilo.

Mkuu wa
Jeshi la Polisi hapa Nchini IGP Simon sirro awaonya vikali askari polisi
wanao kwenda kinyume na sheria na sera za jeshi hilo kwa kukeuka miiko
ya kazi za jeshi la polisi hapa nchini na kuahidi kutowavumilia askari
wote wanao kwenda kinyume na jeshi hilo.
IGP Sirro
ameyasema hayo jijini Arusha alipo kuwa anakabidhi nyumba 6 za askari
polisi katika makao ya askari polisi njiro jijini Hapa nyumba hizo
ambazo ni miongoni mwa nyumba 400 za askari polisi zinazo jengwa nchi
nzima na zilizinduliwa na  Rais Magufuli Mkoani Geita siku kadhaa zilizo
pita.
 
Aidha ameeleza kwamba kufuatia vitendo vingine amabavyo
haviendani na jeshi hilo hato weza kuvivumili atahakikisha wanafukuzwa kazi
akari wote wanao husika na vitendo hivyo na kuchukilia hatua kali za kisheria
na kuwataka askari kuacha tamaa zisizo kuwa na tija.
“Ni mpongeze Rais magufuli kwa kujipatia  shilingi Bilioni 3.5 kwaajili ya kununua
Helkopta maalum kwa jili ya Jeshi letu la polisi na pia Bilion 10 kwaajili ya
kushona sale mpya za askari polisi na mpaka sasa tumeshampata mkandarasi atakae
fanya kazi hiyo yabushonaji sale zetu,pia niwapongeze askari wote ambao
mnafanya kazi kwa uweledi na kuzingatia umoja na ustawi wa nchi yetu kwa
kulinda amani ya raia na mali zao pia hata kupambana na uhalifu kwa kiasi
kukubwa mmeiweka nchi yetu mahali pazuri sasa”. alisema IGP Sirro.
“Ila pia haya yote tunayo yapata kutoka kwa Rais wetu ni
kutokana na kufanya kazi kwa moyo mmoja ma uweledi pia nimpongeze mkuu wa mkoa
wa Arusha Mrisho Gambo amekuwa mstari wa mbele katika maendeleo ya jeshi la
polisi hapa Arusha maana ametusaidia kwa hatua kubwa sana toka ujenzi wa nyumba
za askari zilizo ungua hadi sasa anazidi kutupatia sapoti kubwa sana, Pia RPC
naona yupo vizuri na ndiyo maana hata nyie mnafanya kazi kwa weledi kwa kuiga
mfajo wake mzuri wa utendaji kazi”. aliongeza IGP Sirro.
Kwaupande wake Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Jonathan
Shana ameeleza kwamba nyumba hizo walizo kabidhiwa askari polisi zinatoa hamasa
katika utendaji wa kazi na itachangia kwa kiasi kikubwa askari kuzidi kupenda
kazi zao na kuwa karibu na kazi hata pia itapungiza changamoto ya umbali wa
makazi kwa askari hao.

 
 
 
IGP Siro
amesema mpaka sasa wameshawashikilia askari kadhaa  kwa kesi ya kuwa
uzia sale za jeshi hilo askari wenzio kitu ambacho ni kinyume na
utaratibu wa jeshi hilo na ni kitendo kinacholeta utengano wa kazi ndani
ya jeshi la polisi hapa nchi.


Aidha pia
mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ameipongeza serikali kwa jitihada
hizo madhubuti na kuahidi yeye kama Meenyekiti wa kamati ya ulinzi na
usalma mkoa wa Arusha atahakikisha kila mwaka Jeshi la polisi mkoani
Arusha linapata nyumba sita za makazi kwa askari hao.