Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais,( Muungano na Mazingira) Suleimani
Jafo, akizungumza na wadau wa mazingira katika Mkutano mkuu wa tatu wa
chama cha wataalamu wa mazingira nchini (TEEA) uliofanyika leo Jijini
Dar es Salaam. Mkurugenzi
mkuu wa NEMC Dkt. Samwel Gwamaka akizungumza katika Mkutano mkuu wa
tatu wa chama cha wataalamu wa mazingira nchini (TEEA) uliofanyika leo
Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la
Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Prof. Esnat Chaggu
akizungumza katika Mkutano mkuu wa tatu wa chama cha wataalamu wa
mazingira nchini (TEEA) uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam. Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais,( Muungano na Mazingira) Suleimani
Jafo akiteta jambo na Mwenyekiti wa Chama cha Wataalamu wa Mazingira
(TEEA) Prof.Hussein Sosovere katika Mkutano mkuu wa tatu wa chama cha
wataalamu wa mazingira nchini (TEEA) uliofanyika leo Jijini Dar es
Salaam. Mwenyekiti
wa Chama cha Wataalamu wa Mazingira (TEEA) Prof.Hussein Sosovere
akizungumza katika Mkutano mkuu wa tatu wa chama cha wataalamu wa
mazingira nchini (TEEA) uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Wadau mbalimbali wa mazingira
wakifuatilia Mkutano mkuu wa tatu wa chama cha wataalamu wa mazingira
nchini (TEEA) uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa
Rais,( Muungano na Mazingira) Suleimani Jafo akipata picha ya pamoja na
wadau mbalimbali wa mazingira katika Mkutano mkuu wa tatu wa chama cha
wataalamu wa mazingira nchini (TEEA) uliofanyika leo Jijini Dar es
Salaam.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
NA EMMANUEL MBATILO,DAR ES SALAAM
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa
Rais,( Muungano na Mazingira) Suleimani Jafo, ameliagiza Baraza la Taifa
la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC) kuhakikisha Viwanda vyote
vilivyowekezwa hapa nchini vinafanyiwa tathimini ya Mazingira.
Waziri Jafo ametoa agizo hilo leo
Jijini Dar es Salaam wakati akizungumza katika Mkutano mkuu wa tatu wa
chama cha wataalamu wa mazingira nchini (TEEA) ambapo amesema kuwa
Viwanda ambavyo bado havijafanyiwa tathimini ya Mazingira kufanyiwa
hivyo mara moja.
Aidha amemtaka mkurungenzi wa NEMC
kutoa tangazo maalumu kwa wawekezaji wote wanaposajili miradi mbalimbali
kuhakikishe wanaanza na mchakato wa tathimini ya Mazingira huku akipiga
marufuku kwa wawekezaji hao kuwatumikisha wataalamu bila kuwalipa.
Amesema wataalamu zaidi ya 1,000
Wamepatiwa usajili ambao unawawezesha kufanya tathimini ya athari za
mazingira lakini wataalamu 250 pekee ambao ni sawa na asilimia 25% ya
wote waliosajiliwa ndio wanafanyazi.
“Hata hapa kwenye mkutano
nimeangalia hao wataalamu 250 waliohai kazini wengi wao hawajahuhudhulia
mkutano huu ambapo watakosa fursa ya kujadili kanuni mpya za
mazingira,kupitia mfumo mpya wa kimtandao wa kusajili vyeti vya
mazingira kwa wahitaji kwahiyo wachache waliohudhilia watapata manufaa
makubwa”Alisema Jafo.
Katika hatua nyingine Jafo
amewaagiza wataalamu wa Mazingira kutumia Taaluma zao kuangalia njia
bora ya kudhibiti athari ya madini ya zebaki ili kuepuka madhara
yanaweza kujitokeza.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama
cha Wataalamu wa Mazingira (TEEA) Prof.Hussein Sosovere amesema kuna
tathimini 5,000 zimeandikishwa lakini tathimini 55 pekee ndio zimepatiwa
vyeti,hivyo inaonyesha wazi jinsi wataalamu wa mazingira wanaweza
kuchangia maendeleo ya Taifa kwa kuhakikisha Shughuli za maendeleo
haziharibu mazingira.
Nae Mkurugenzi mkuu wa NEMC Dkt.
Samwel Gwamaka amesema kuwa tangu kuanza kwa usajili kwa njia ya mtandao
imesaidia kuondoa ucheleweshwaji usiokuwa na ulazima pia imesaidia
kuondoka watu wanaojiita wasaidizi elekezezi maarufu kama Makanjanja,
wakati hawajasajiliwa na mamlaka husika.
Hata hivyo wawekezaji wametakiwa kuzingatia tathimini ya Mazingira kabla ya kuanzisha miradi yao hapa nchini.