Jeshi la polisi dodoma lakanusha kumpiga mwananchi


Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.

Jeshi
la Polisi mkoa wa Dodoma limekanusha kuhusika na  taarifa za kumpiga
Raia mmoja ajulikanaye kwa jina la   Elisha Hezron Wanjara[39] na kudai
kuwa taarifa hizo sio za kweli na zimerushwa na Baadhi ya Vyombo vya
Habari bila kufanyiwa uchunguzi.

Akizungumza
na Waandishi wa Habari jijini Dodoma,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma
Girres Muroto amesema Tarehe 7,oktoba ,2019 Mwandishi wa Habari kupitia
GLOBAL TV ONLINE ,Bw.Mohamed Zengwa alirusha katika mitandao ya kijamii
habari ya mtu mmoja aitwaye ELISHA HEZRON WANJARA[39]MJITA Fundi Ujenzi
wa Barabara katika kampuni ya STECOL inayofanya kazi za ujenzi hapa
Dodoma  ambapo taarifa hizo zilidai mtu huyo alipigwa na Jeshi la
Polisi.
Kamanda
Muroto amesema katika taarifa hiyo ilifafanua kuwa Bw.WANJARA alipigwa
na askari polisi wa doria na kuporwa simu pamoja na fedha kiasi cha
Tsh.Elfu 70 na kupakiwa kwenye gari la polisi na kuwekwa kwenye mahabusu
ya Polisi  na baadaye kuachiliwa huru bila matibabu,bila kurejeshewa
simu na pesa zake  na alikwenda kwa mkuu wa wilaya na kuongea naye juu
ya jambo hilo na kurusha mtandaoni.
Hata
hivyo,Kamanda Muroto amesema habari hiyo ni ya uongo na haina ukweli
wowote  hivyo Bw.WANJARA alisema  uongo ,hakuibiwa simu ,hakuporwa fedha
wala kupigwa na askari  kama alivyojieleza kwa mwandishi wa habari
mbele ya mkuu wa wilaya wa  Dodoma mjini.
Aidha,Kamanda
Muroto ameelezea Ukweli wa tukio kuwa ,siku ya Tarehe 6/10/2019 
Bw.Elisha Hezron Wanjara na Mwenzake mmoja aliyejulikana kwa jina la
utani NGINJANGINJA walikwenda nyumbani kwa Paulo Mkazi wa Mtaa wa
IPAGALA akitafuta chumba cha kupanga na walimchukua mwenyeji wao
wakaenda kunywa pombe za kienyeji nyumbani kwa mama Eliza.
Kamanda
Muroto ameendelea kufafanua kuwa ,wakati wanaendelea kunywa pombe
,Bw.WANJARA alimpatia Simu Bw.PAULO CHIPAGALA awapige picha na aliwapiga
picha mbalimbali wakati wanakunywa pombe na baada ya kulewa walianzisha
ugomvi mkubwa  na kupigana kwa muda mrefu.
Hivyo,waliumizana
na wote wakasambaratika eneo hilo  na haikujulikana kila mmoja
alikokwenda  na simu aliendelea kubaki nayo PAULO CHIPAGA  aliyepewa na
mwenye simu kabla ya kulewa na kupigana.
Kamanda
Muroto amebainisha ,usiku wa saa 3:45 Elisha Wanjara aliokotwa na
wapita njia na kumpeleka kituo cha polisi  Central Dodoma akiwa amelewa
pombe ,hajitambui na ana majeraha ya kupigwa  na aliandikiwa PF3 ili
aende kutibiwa  na waliompeleka ni watu walewale waliomleta kituoni.
Baada
ya kurudisha PF3 aliyopewa kituo  cha Polisi ,kulipopambazuka alikwenda
kwa mkuu wa wilaya ya Dodoma ,akatoa taarifa na maelezo ya uongo kuhusu
jeshi la polisi akisingizia askari kumpiga ,kupora simu na fedha.
Kamanda
Muroto amevieleza vyombo vya habari kuwa,Jeshi la polisi limefanya
uchunguzi kuhusu tukio hilo  na kubaini ukweli na mafanikio ambayo ni
Bw.WANJARA hakukamatwa na askari polisi kwenye msako,simu
haikuporwa,bali alimpatia PAULO CHIPAGA na ilipatikana kutoka kwa
CHIPAGA,Majeraha aliyopigwa ni kutokana ugomvi wake na mwenzake.
Mambo
mengine yaliyobainishwa na Jeshi la polisi kuwa ni hakuporwa
Tsh.70,000,na siku ya tukio aliomba Tsh.5000 kutoka kwa JOHN NTALE
Msimamizi wake wa kazi,amewasingizia askari polisi na kutoa maelezo ya
uongo kwa mkuu wa Wilaya  na kuudanganya umma wa Tanzania na
kulichafulia jeshi la Polisi kwa tukio la kuunda na Maneno ya uongo.
Kwa upande wake Bw.WANJARA amehojiwa na amekiri kuwa alitoa taarifa za uongo na alikuwa amelewa pombe.
Kutokana
na tukio hilo,mtuhumiwa anashikiliwa na jeshi la polisi na amefunguliwa
mashtaka kwa kutoa taarifa za uongo  na atafikishwa mahakamani hivyo
kamanda Muroto ametoa onyo kwa wanaotumia vibaya ofisi za serikali kutoa
taarifa za uongo  na kuwataka wanahabari kuzifanyia uchunguzi na subira
habari kabla ya kuzirusha ili kuondoa mkanganyiko katika jamii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *