Jeshi la polisi mkoa wa shinyanga linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kumnyonga hadi kufa mzee mwenye umri wa miaka 85, mkazi wa kitongoji cha nyambui kata ya tinde

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga linawashikilia watu wawili wanaosadikiwa
kuhusika na tuhuma za  kumnyonga hadi
kufa M
zee Masanja Tungu Masesa mwenye umri wa Miaka
85
, Mkazi wa kitongoji na kijiji cha Nyambui kata
ya Tinde Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa
kitongoji cha Nyambui  Bwana Masesa Mkata
tukio hilo
limetokea usiku wa
kuamkia  Oktoba 21,2023
katika
kijiji cha Nyambui kata ya Tinde.

“Mnamo
muda wa saa mbili usiku mzee Masanja alikuwepo tu nyumbani na mjukuu wake baada
ya kula chakula cha usiku waliingia ndani kulala kila mtu kwenye chumba chake
basi yule kijana badaye alisikia babu yake kama vile anagombana na mtu furani
alipoenda alikutana na mwanaume amevaa nguo za kujifunika uso kama vile ninja
likamkalipia kwa kumtishia akarudi ndani kulala, baada ya kumaliza mwanaume
huyo alichukua unga, mahindi akachukua na godolo likaondoka yule kijana
lilimwambia asipige kelele kuja kuangalia asubuhi akakuta yule mzee amenyongwa”.amesema
Mwenyekiti Masesa

Kwa upande wake kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kamishna
msaidizi wa Polisi Janeth Magomi ame
thibitisha kukamatwa kwa  watuhumiwa hao wawili ambao wanadaiwa kuhusika na tukio hilo.

‘Tunaendelea na
upelelezi lakini hata hivyo katika upelelezi huu tayari tumewakamata watu
wawili lakini bado tunaendelea na uchunguzi 
ili kubaini chanzo cha tukio hilo”.amesema kamanda Magomi