Jeshi la polisi shinyanga kuendelea na uchunguzi katika tukio la mtoto wa miaka 12 mwanafunzi darasa la nne ndembezi kujinyonga

 

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Mwili wa mtoto aliyesadikiwa kujingonga hadi kufa mwenye
umri wa miaka 12 anayetambulika kwa jina la Elisia Katondo mkazi wa mtaa wa
Ndembezi Mwanoni katika Manispaa ya Shinyanga
umesafirishwa leo kwenda Mkoani Kigoma kwa ajili ya
mazishi.

Akizungumza Baba mlezi wa marehemu huyo Bwana
William Bayona
amesema mwili
huo umesafirishwa leo Jumanne Oktoba 17,2023kutoka Shinyanga kuelekea mkoani
Kigoma nyumbani kwa wazazi wa marehemu,ambapo  baada ya kuwasili mkoani humo taratibu za mazishi
zitafanyika.

Tukio la kujinyonga kwa Mtoto
huyo limetokea Oktoba 15, Mwaka huu 2023 majira ya usiku.

Kwa
upande wake Mjumbe wa serikali ya mtaa wa Ndembezi Mwanoni Joice Tambwe amesema
taarifa za tukio hilo alizipokea majira ya saa tatu usiku Oktoba 15,2023.

Aidha
kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kamishna msaidizi wa Polisi Janeth
Magomi amesema jeshi hilo linaendelea na uchunguzi ili kubaini chanzo cha tukio
hilo.

Elisia
Katonda mwenye umri wa miaka 12, alikuwa anasoma darasa la nne shule ya msingi
Ndembezi Manispaa ya Shinyanga.