Jiji la arusha latapakaa uchafu kila kona,hofu ya kuibuka magonjwa ya mlipuko yatanda

Baadhi ya marundo ya Taka katikati ya Jiji la Arusha kama yalivyokutwa
na kamera ya matukio jijini Arusha katika eneo la Kata ya Kaloleni
jijini hapa picha na Ahmed Mahmoud Arusha.
Pichani ni rundo la Taka lililokutwa pembezoni mwa uwanja wa Sheikh Amri
Abeid na kamera ya matukio jijini Arusha picha na Ahmed Mahmoud Arusha

Na Ahmed Mahmoud Arusha

Halmshauri ya Jiji la Arusha
inatuhumiwa kwa kushindwa kuzoa Taka katika jiji la Arusha kwa kipindi
cha mwezi moja Sasa hali inayoonyesha kuhatarisha kupelekea  kuzuka jwa
magonjwa ya milipuko.
Kwa
muda wa wiki takribani mbili chunguzi uliofanywa na mwanahabari hili
kwenye kata mbalimbali za jiji la Arusha imekutana na msongamano wa
marundo ya Taka kwenye Kata za Kaloleni Sinon Sokon 1 na Unga Ltd yakiwa
yamezagaa baada ya magari kushindwa kuchukuwa taka hizo.
Hata
hivyo Wafanyakazi wa usafi kwenye Kata za jiji hilo ikiwemo Kaloleni
wamekuwa wakifanya usafi wakipangiwa maeneo makubwa hali inayowawia
vigumu kutekeleza majukumu yao ya kila siku.
Akiongea
mmoja wa Wafanyakazi hao aliekataa kutaja jina alisema kuwa utaona Mimi
naanzia kufanya usafi kuanzia Stand Ndogo Hadi maeneo ya Polisi na
kipato ni kile kile lote hilo ni eneo langu naiomba mamlaka kuangalia
hilo.
Hata hivyo sehemu
kubwa ya mitaro imejaa udongo hali inayopelekea maji kujaa barabarani
hususani nyakati hizo za mvua zinazoendelea kunyesha kwenye maeneo
mbalimbali mkoani hapa hali inayoonyesha maagizo ya waziri wa Tamisemi
Suleiman Jaffo alitoyatoa kwa uongozi wa Jiji la Arusha kutotekelezwa
kwa kipindi chote tokea mwaka Jana alipotembelea kuona ujenzi wa
barabara ya dampo hadi Mrombo.
Kwa
upande wake alipotakiwa kujibu suala hilo Afisa Mazingira wa Jiji la
Arusha James Lobkok alijibu kwa ufupi kuwa atapiga baadae nae bibi Afya
wa kata ya Kaloleni alipopigiwa simu   ili kuweza kutoa majibu alisema
kuwa atafutwe saa sita mchana atakuwa tayari kujibu suala hilo.