Na Mapuli Misalaba, Shinyanga
Jumuiya ya wazazi kupitia chama cha mapinduzi CCM Wilaya ya
Shinyanga mjini imekemea suala la ukatili ikiwemo ubakaji na ulawiti kwa watoto
huku ikiziomba mamlaka husika kuchukua hatua kali kwa watu wanaobainika kufanya
vitendo hivyo.
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Shinyanga mjini Bwana Fue Mrindoko kwenye ziara ya kutembelea na
kukagua uhai wa jumuiya ya wazazi kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga
ambapo pamoja na mambo mengine amekemea suala la ukatili kwa watoto.
Mwenyekiti huyo ameiomba jamii hasa wazazi kushirikiana katika
kutokomeza vitendo vya ukatili ambapo ameziomba mamlaka kuchukua hatua za
kisheria kwa watu wanaobainika kufanya vitendo vya ubakaji na ulawiti kwa
watoto na kwamba hali hiyo inachangia mmomonyoko wa maadili kwenye jamii na
Taifa kwa ujumla.
“Mambo
ya kunajisi watoto, mambo ya kulawiti watoto ni jambo ambalo tunalikemea sana
hatulihitaji hilo na sisi kama wazazi hilo ni suala la kulihubiri kila mtu
kwamba watoto wetu hawa wanaochezewa wale ambao wanahusika na vitendo hivyo
wachukuliwe hatua mara moja kama wazazi tusiukumbatie uovu huo”.amesema
Mwenyekiti Mrindoko
Katika hatua nyingine
Mwenyekiti huyo ameishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuleta
fedha nyingi kwa ajili ya maendeleo.
“Katika ziara hii tumeshuhudia miradi ya maendeleo inaendelea kutekelezwa
mfano hata hili daraja linalounganisha kata ya Ibinzamata na Kitangiri ujenzi
wake unaendelea vizuri na tunatarajia hadi ifikapo Juni 1,2023 daraja hili
ambalo limekuwa kero kwa muda mrefu litaanza kutumika”,amesema Mrindoko.
“Ujenzi
wa daraja la Kitangili unaridhisha na mwezi Juni wananchi wataanza kupita pale.
Mradi huu unaendelea vizuri”,amesema.
Kwa upande wake mjumbe wa kamati ya utekelezaji
jumuiya ya wazazi Wilaya ya Shinyanga mjini Mhandisi James Jumbe amesisitiza
jamii hasa wazazi kuepukana na mazingira yanayosababisha ukatili kwa watoto ili
kuimarisha usalama wao.
Katibu wa jumuiya ya wazazi Wilaya ya Shinyanga mjini Bi.
Doris Kibabi amesema ni wajibu wa kila mzazi au mlezi kutekeleza wajibu wake wa
mtoto katika malezi bora ili kuandaa Taifa bora la vijana wasomi.
Aidha katibu huyo amesisitiza matawi yote kwenye kata
jumuiya ya wazazi Wilaya ya Shinyanga mjini kuongeza wanachama wapya ili
kuendelea kuimarisha jumuiya hiyo.
Kamati ya utekelezaji jumuiya ya wazazi Wilaya ya
Shinyanga mjini leo Mei 12,2023 imeendelea na ziara yake ya kutembelea na
kukagua uhai wa jumuiya kwenye kata ambapo leo pamoja na mambo mengine wametoa
msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo chakula kwenye kituo cha kituo cha kulelea watoto cha Brother of Charity
kilichopo Kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga
Kamati ya utekelezaji jumuiya ya wazazi Wilaya ya
Shinyanga mjini ikitembelea na kukagua ujenzi wa daraja la
Kitangili leo Ijumaa Mei 12,2023 ikiwa ni sehemu ya ziara ya kutembelea na
kukagua uhai wa jumuiya kwenye kata katika Wilaya hiyo ya Shinyanga mjini.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Kata ya Kitangili
Zawia Hassan Mpanda akizungumza kwenye kikao hicho leo Ijumaa mei 12,2023.
Mjumbe wa kamati ya utekelezaji Jumuiya ya Wazazi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini
Mhandisi James Jumbe akizungumza kwenye kikao hicho leo Ijumaa Mei 12,2023.
Mjumbe wa kamati ya utekelezaji Jumuiya ya Wazazi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Mhandisi James Jumbe akizungumza kwenye kikao hicho leo Ijumaa Mei 12,2023.
Mjumbe wa kamati ya utekelezaji Jumuiya ya Wazazi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Mhandisi James Jumbe akizungumza kwenye kikao hicho leo Ijumaa Mei 12,2023.
Katibu wa jumuiya ya wazazi Wilaya ya Shinyanga mjini Bi.
Doris Kibabi akihamasisha viongozi kuongeza na kusajiri wanachama wapya kata
hiyo ya Kitangili leo Ijumaa Mei 12,2023.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya
Wazazi Wilaya ya Shinyanga mjini Bwana Fue Mrindoko akizungumza kwenye kikao hicho
leo Ijumaa Mei 12,2023.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya
Wazazi Wilaya ya Shinyanga mjini Bwana Fue Mrindoko akizungumza kwenye kikao hicho
leo Ijumaa Mei 12,2023.