Kanyasu awahakikishia wajerumani kuwa ujenzi wa bwawa la kufua umeme la julius nyerere limezingatia mazingira

Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akiwa kwenye picha ya pamoja kwenye na
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Mazingira, Uhifadhi wa Maliasili na
Usalama wa Nyuklia kutoka Ujerumani Wengine ni baadhi ya watumishi wa
wizara ya maliasili na Utalii.
Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akimkabidhi zawadi ya jarida la Utalii
la ” Tanzania Unforgettable” mmoja  wa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya
Mazingira, Uhifadhi wa Maliasili na Usalama wa Nyuklia kutoka Ujerumani,
Mhe. Stewrar Genejip  mara baada ya kumalizika kwa kikao
kilichofanyika  katika ukumbi wa Wizara ya Maliasili na Utalii jijini
Dodoma.
Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akizungumza na Wajumbe Kamati ya Bunge
ya Mazingira, Uhifadhi wa Maliasili na Usalama wa Nyuklia kutoka
Ujerumani wakati wa kikao c ha kujadili masuala ya Uhifadhi katika 
kikao kilichofanyika  katika ukumbi wa Wizara ya Maliasili na Utalii
jijini Dodom. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Dkt. Maurus
Msuha.
Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akimkabidhi zawadi ya jarida la Utalii
la ” Tanzania Unforgettable” kwa Kiongozi wa ujumbe wa Kamati ya Bunge
ya Mazingira, Uhifadhi wa Maliasili na Usalama wa Nyuklia kutoka
Ujerumani, Mhe. Sylvia Kotting- Uhl mara baada ya kumalizika kwa kikao
kilichofanyika  katika ukumbi wa Wizara ya Maliasili na Utalii jijini
Dodoma.
Baadhi ya Wajumbe
waKamati ya Bunge ya Mazingira, Uhifadhi wa Maliasili na Usalama wa
Nyuklia kutoka Ujerumani wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii, Mhe, Constantine Kanyasu wakati wa kikao kilichofanyika jijini
Dodoma
(PICHA NA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII)
********************************
Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu amesema nia ya Serikali ya ujenzi wa
bwawa  la kufua umeme la Julius Nyerere iko pale pale na ujenzi wake
unaendelea kwa kasi huku ukizingatia masuala ya Uhifadhi katika Pori la
Akiba la Selous.
Akizungumza leo na Wabunge wa
Kamati ya Bunge ya Mazingira, Uhifadhi wa Maliasili na Usalama wa
Nyuklia kutoka Ujerumani Mhe. Kanyasu  amesema Tathmini ya Athari kwa
Mazingira imefanyika na kuonyesha kuwa ujenzi huo ni salama katika
shughuli za Uhifadhi.
“Serikali ya Awamu ya Tano
inatekeleza mradi huu kwa kutumia fedha zake kutoka vyanzo vya ndani.
Mradi huu utachukua eneo la ukubwa wa kilomita za  mraba 1,250 ambalo ni
sawa na asilimia tatu (3%) tu ya eneo lote la pori la akiba selous
lenye ukubwa wa kilomita za mraba 50,000.” Mhe. Kanyasu alisisitiza.
Mhe. Kanyasu amesema  kiwango
cha umeme cha megawati 2,100 kitakachozalishwa katika gridi ya Taifa
itasaidia kwa kiasi kikubwa kuokoa misitu inayokatwa kwa kasi kwa ajili
ya nishati ya mkaa na kuni.
Aidha, Mhe. Kanyasu amewaeleza
Wabunge hao kuwa ujio wa Bwawa hilo la Umeme limepelekea sehemu ya Pori
la Akiba la Selous kupandishwa hadhi na kuwa Hifadhi ya Tiafa ya Julius
Nyerere ambapo kufuatia hali hiyo ulinzi wa wanyamapori katika Hifadhi
hiyo utakuwa madhubuti zaidi na ilivyokuwa mwanzo.
Katika hatua nyingine Mhe.
Kanyasu amewaeleza Wabunge hao kuwa Serikali ya Tanzania imelichukua
suala la mabadiliko ya tabia ya nchi kwa uzito unaostahili na kwa
kutambua athari zake kwa mwaka huu imepandisha hadhi mapori ya akiba
manne na  kuwa Hifadhi za Taifa na hivyo ulinzi wake wa Hifadhi hizo
umeongezeka maradufu.
Kwa upande wake Kiongozi wa
ujumbe huo Mhe. Sylvia Kotting- Uhl ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa
mageuzi makubwa yanayofanyika katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya
Tano katika masuala ya Uhifadhi  na kuahidi ushirikiano na nchi
yake katika kujenga uwezo katika nyanja za kusimamia na kudhibiti taka
za kielektroniki, Uzalishaji wa Umeme wa jua na kutoa mwaliko kwa ujumbe
wa Tanzania kutembelea Ujerumani.
Aidha, Mhe.Sylvia amesema
licha ya ujenzi wa Bwawa la Umeme la Julius Nyerere bado wataendelea
kuisaidia Serikali ya Tanzania katika masuala ya Uhifadhi kufuatia
juhudi kubwa za Serikali ya awamu ya tano ya kuendelea kutunza na
kuhifadhi maeneo yasiweze kuharibiwa na shughuli za kibinadamu.