Kata ya ndala yaadhimisha siku ya wanawake diwani zamda atoa msaada kwa wazee wasiojiweza” dc samizi akemea wimbi la ulawiti na ubakaji

Na Mwandishi wetu 

Kata ya Ndala Manispaa
ya Shinyanga imeazimisha sherehe za siku ya wanawake kwenye kata huku
ikifanyika na kutoa msaada kwa wazee wasiojiweza kwenye kata hiyo.

 Hafla hiyo imefanyika
tarehe 01/04/2023 katika viwanja vya soko la Ndala lililopo Manispaa ya Shinyanga ambapo pamoja na mambo mengine wamepanda miti 250.

Akiongea mbele ya
wananchi hao Diwani wa kata hiyo Mhe. Zamda Shaban amewahakikishia wakazi
wa  kata hiyo kuwa sherehe hizo zitakuwa
zinafanyika kila Mwaka ili kuendeleza umoja, mshikamano na upendo.

” Ndugu zangu Wana Ndala leo ni siku
maalumu, tuliyoitenga  kwa ajili ya kuzungumza,kucheua na kupeana zawadi
kidogo, hivyo tutakua tunafanya kila mwaka ili kujenga umoja kwenye kata
yetu”

Aidha akitoa taarifa kwa mgeni rasmi ambae
alikua Mkuu wa wilaya ya Shinyanga mheshimiwa Johari Samizi diwani huyo alisema

” _Mheshimiwa hapa tuna soko letu la kata
ya Ndala, Hili soko Lina zaidi ya miaka 20 halifanyi kazi,wamama walikuja hapa
wakawekeza,wakajenga vizimba, na vibanda lakini halijafanya kazi, hivyo
tunaomba ulifatilie ili tupate ufumbuzi”_
alisema Diwani Zamda

 Kwa upande wake Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga
 Mhe. Johari
Samizi kabla ya shughuli hiyo alipata nafasi ya kupanda mti wa mwembe eneo
ofisi ya kata ya Ndala.

 DC Samizi pamoja na mambo mengine wakati
akizungumza na wananchi amekemea
 vikali
suala la ulawiti na kuwataka wazazi kulea watoto katika maandili mema ili
kuandaa Taifa bora.

“Ndugu zangu, wazazi wenzangu tuna jukumu
kubwa Sana la kuilinda jamii, na ulinzi wa mtoto unaanza nawewe mzazi, hivyo
niwaoambe wazazi wote tujitahidi kuwalinda watoto, tufatilie shule wanazosoma,
tufatilie mienendo yao pia tusiruhusu watoto kuangalia katuni zisizofaa, na
zisizo na maadili kwenye jamii yetu”.
amesema DC Samizi

 Sherehe hizo
zilipambwa na utolewaji wa zawadi na misaada mbali mbali  kwa wazee 110
kutoka kata ya Ndala yote na zawadi hizo zlikua ni unga kilo tano kwa kila
mzee,sukari,sabuni na mche mmoja wa mti wa mwembe

 Akizungumza kwa
niaba  ya wazee wote waliopata msaada huo Mama Juma mkazi wa mtaa wa
Mwabundu, alisema

“Namshukuru Sana Diwani Zamda kwa
kutukumbuka sisi wazee wa Ndala, haswa wamama hatuna chakumlipa na tunaahidi
kumuombea kwa Mungu azidi kumbariki maradufu,na alipotoa azidi kuongezewa,
alisema mama Juma aliyepata msaada huo”

Kauli mbio ya Mwaka huu inasema “NDALA BILA
UDUMAVU WA WATOTO NA CHAKULA SHULENI INAWEZEKANA”