Kichanga chaokotwa mto kanoni

Na
Clavery Christian Bukoba Kagera.
Wakazi wa mtaa wa Buyekera manispaa ya Bukoba mkoani
Kagera wameshuhudia tukio la kinyama 
baada ya mwili wa kichanga kuonekana ukielea katika mto Kanoni.
Wakizungumzia tukio hilo la kinyama mashuhuda hao
waliofika katika eneo la tukio wamesema kuwa wakiwa wanapita katika eneo hilo jana Mei 8, 2020 katika daraja hilo waliona mwili wa kichanga hicho kikiwa kinaelea juu ya maji 
Katika tukio hilo la kusikitisha, uongozi wa Serikali ya mtaa wa Buyekera umedai kusikitishwa na kitendo cha kifo cha kichanga hicho na kwamba watafanya uchunguzi kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi ili kuweza kubaini aliyefanya uhalifu huo.

Mwenyekiti wa mtaa wa Buyekera lilipotokea tukio
hilo Justinian Kamugisha amesema kitendo hicho ni cha kinyama  na kuwataka wananchi
kut
oa taarifa kwa mamlaka zinazohusika pindi wanapobaini watu wanaohusika na
vitendo hivyo.

Akizungumzia tukio hilo mkuu wa kikosi cha zimamoto na
uokoaji mkoa wa Kagera  Hamis Dawa
amesema kuwa wamepata taarifa kutoka kwa wananchi juu ya kuonekana kwa kichanga
hicho kulazimika kwenda kuopoa mwili huo na kuwa baada ya kuupoa umepelekwa
katika hospitali ya Rufaa ya mkoa kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Hata hivyo wakazi hao wamelaani tukio hilo huku
wakiomba uchunguzi ufanyike ili kumbaini aliyehusika na unyama huo.