Kuelekea mwisho wa mwaka – madereva watakiwa kuzingatia sheria za barabarani na kuacha visingizio kuwa watu wanatoa kafara

Ally Nurdin (mwenye kipaza sauti) ni Mkurugenzi wa Idara ya Elimu Mawasiliano na Habari kwa Umma.

Na.Vero Ignatus.
Madereva
wa magari ya abiria wameaswa kukagua magari yao kabla ya kuanza safari
,sambamba na kuzingatia sheria ,michoro,kanuni,na alama za usalama
barabarani ili kuepusha mwendo kasi na kusababisha ajali,hivyo kupelekea
kusingizia kwamba watu wanatoa kafara

Hayo
yamesemwa na Mkurugenzi wa Idara ya elimu mawasiliano na habari kwa
umma( RSA) Ally Nurdin ,kwamba katika kipindi cha kuelekea sikukuu za
mwisho wa mwaka ,waangalie matumizi sahihi ya barabara wakizingatia kuwa
ni kipindi cha mvua ,kwani tayari watu walishashuhudia ajali
zilizogharimu uhai hata kusababisha vifo, majeraha makubwa na ulemavu wa
kudumu.

Nurdin amewahusia
wamiliki wa magari binafsi haswa madogo ,kuwa makini katika kipindi
hiki ambacho ,wanakuwa safarini kuelekea katika mapumziko ya sikukuu za
mwisho wa mwaka, kwani kuendesha gari mjini haiwapi fursa ya wao
kuendesha safari ndefu hivyo ni bora wafute dereva 

”Wenye
magari madogo wengi wamekuwa wakisafiri na magari yao,kumiliki gari na
kuendesha mjini haikupi kibali cha wewe kusafiri safari ndefu,safari
ndefu inahitaji uzoefu wa kutosha,kama hujazoea kusafiri safari ndefu
nashauri utafute dereva akuendesha” 

Aidha
amewataka wazazi wawapo safarini  kuwafunga watoto mikanda pia
wasiruhusu watoto  wao kurukaruka na kucheza kwenye gari wakati wa
safari jambo ambalo ni hatari

”Wote
waliopo kwenye gari wafunge mkanda na tabia ya kuwaacha watoto
kurukaruka na kucheza ndani ya gari ni wakati wa safari ni hatari,pia
acheni tabia ya kujazana kwenye gari kisa huyu ni binamu ,sijui mtoto wa
mjomba ,baba mdogo epukeni hilo”alisisitiza Ally 

Pia
ametoa wito kwa abiria kuwa makini wawapo safarini kwa kutokupokea
chakula cha aina yeyote kwa abiria mwenzake asiyemfahamu ,kwani anaweza
kupata madhara ya kiafya au kuibiwa.

Sambamba
na hayo amewataka watembea kwa miguu pia kuzingatia alama na michoro ya
barabarani  nyakati nzote,na katika kipindi hiki cha sikukuu za mwisho
wa mwaka waepuke kutumia vilevi kupita kiasi ambapo inaweza kuwapelekea
kulala pembezoni mwa barabara na wao wakuwa chanzo kimojawapo cha ajali .