Kupinga unyanyapaa chachu ya kupunguza maambukizi mapya

Spika wa bunge la Tanzania Job Ndugai akifungua Kongamano la siku mbili la viongozi wa dini watu wanaoishi na maambukizi lililoandaliwa na Bunge na Baraza la watu wanaoishi na maambukizi ya ukimwi Nacopha iliofanyika jijini Arusha leo 

Na Ahmed Mahmoud Arusha

Taarifa sahihi za unyanyapaa zikifanyiwa kazi itasaidia kuwafichua watu wenye maambuzi mapya na kuendeleza vita ya kupigana na Ugonjwa wa ukimwi nchini.
Pia Baraza la watu wanaoishi na virusi vya ukimwi Nacopha kupitia mradi wa hebu tuyajenge kwa msaada wa watu wa Marekani pamoja na Bunge la Tanzani

a wameendesha kongamano la viongozi wa dini lenye lengo la kuona namna ya kuondoa unyanyapaa kwa watu wanaoishi na maambukizi ya ukimwi miongoni mwa jamii yetu hapa nchini.

Akiongea kwenye Kongamano hilo la siku mbili lililoandaliwa na taasisi hiyo kwa kushirikiana na Bunge Afisa Mtendaji Mkuu wa Nacopha Deogratius Rutatwa alisema kuwa suala la unyanyapaa limekuwa kwa muda mrefu kwenye jamii yetu hivyo ni busara sasa kuchukuwa hatua za kuanza kulidhibiti kwa lengo la kuliondoa tatizo hilo.
Alisema kuwa vyombo vya habari viangalie Sana suala zima la uripoti wa taarifa za watu wenye maambukizi ya ukimwi badala ya kueleza kwa kusema mtu mwenye VVU hii teyari unakuwa umemnyanyapaa hivyo taarifa zao zisiwe kwenye eneo la unyanyapaa ambao ni ubaguzi ambao ni dhambi.
Kwa upande wake Katibu mkuu wa CPCT nchini Mchngaji Elingarami Munisi alisema kuwa Serikali ifikirie upya marekebisho ya kuhusu matibabu ya bima ya Afya hususani Ugonjwa wa Figo.
Nae Mbunge wa viti Maalum na mjumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya masuala ya ukimwi,na kifua kikuu Salma Kikwete aliiomba jamii kuwepo kwa ushirikiano wa kutosha juu ya kuripoti matukio ya unyanyapaa hasa katika suala zima la ubakaji kwa watoto.
Aliongeza kuwa kutotoa taarifa za ubakaji wanaofanyiwa watoto ni aibu kubwa na huo ni unyanyapaa hivyo ni wajibu wa kila moja kwa nafasi yake kuhakikisha wanakuwa walinzi wa watoto na kuripoti matukio katika mamlaka husika.
“Suala zima la unyanyapaa linakuwepo kutokana na kutokuwa na elimu sahihi jinsi ya kuwalinda na kuwatete watu wanaoishi na maambukizi ya ukimwi hivyo elimu zaidi inahitajika kutolewa ili kuwalinda na hatimaye kuweza kupata haki zao”alisema