Latra yaendesha zoezi la kukamata magari yasiyokuwa na leseni pamoja na yale yanayopita barabara zilizokatazwa.

 Pichani ni moja ya gari la abiria Hiace kama inavyoonekana likiwa limekatiza kwenye barabara hiyo ambayo hayaruhusiwi kupita magari hayo,lenye Ruti ya Ngusero/Ngaramtoni.Picha na Vero Ignatus.
 Moja ya  gari la abiria Hiace kama inavyoonekana likiwa limekatika kwenye barabara hiyo ambayo hayaruhusiwi kupita magari Hayo,lenye Ruti ya Chekereni Ngaramtoni
Pichani ni moja ya gari la abiria Hiace kama inavyoonekana likiwa limekatika kwenye barabara hiyo ambayo hayaruhusiwi kupita magari hayo,lenye Ruti ya Morombo/Ngaramtoni.
Muonekano wa Barabara inayokataliwa kupita magari hayo ya Abiria ya Rexona Road yenye urefu wa mita 300, inayokwnda kuungana na Nairobi Rodi 

Na Vero Ignatus, Arusha


 Pichani ni moja ya gari la abiria Hiace kama inavyoonekana likiwa limekatika kwenye barabara hiyo ambayo hayaruhusiwi kupita magari Hayo,lenye Ruti ya Ngusero/Ngaramtoni.Picha na Vero Ignatus.
 Moja ya  gari la abiria Hiace kama inavyoonekana likiwa limekatika kwenye barabara hiyo ambayo hayaruhusiwi kupita magari Hayo,lenye Ruti ya Chekereni Ngaramtoni
Pichani ni moja ya gari la abiria Hiace kama inavyoonekana likiwa limekatika kwenye barabara hiyo ambayo hayaruhusiwi kupita magari hayo,lenye Ruti ya Morombo/Ngaramtoni.
Muonekano wa Barabara inayokataliwa kupita magari hayo ya Abiria ya Rexona Road yenye urefu wa mita 300, inayokwnda kuungana na Nairobi Rodi 

LATRA YAENDESHA ZOEZI LA KUKAMATA MAGARI  YASIYOKUWA NA LESENI PAMOJA NA YALE YANAYOPITA BARABARA ZILIZOKATAZWA.


Na Vero Ignatus, Arusha

Mamlaka ya usimamizi ya usafiri nchi kavu Latra imeendesha  zoezi la ukamataji wa magari ya abiria yanayopita barabara ambazo zimekatazwa haswa katika eneo la Ngarenaro Jijini Arusha.

Msafiri Nihuka Afisa wa Latra mkoani hapa amesema imewalazimu kufanya hivyo kwasababu barabara hiyo ni makazi ya watu na magari hayo yakipita yanaweza kusababisha ajali kwa watembea kwa miguu au kwa watoto ambao wanaoishi katika mtaa huo.

Amesema hadi  sasa jumla ya magari tisa ya abiria yamekamatwa na kupigwa faini,Faini,pamoja na magari 10 ya abiria ambayo hayana leseni  ambapo amesema  kuwa zoezi hilo ni endelvu la kuwakamata
madereva  wazembe wanaokaidi amri hiyo.

Aidha Nihuka ametoa onyo kwa madereva watakao kaidi agizo hilo na kusema kuwa Latra itawachululia hatua za kisheria kwa kukiuka masharti ya leseni.

Mwenyekiti mstaafu wa TCA  Amosi Kimaro amesema kuwa  wao kama wakazi wa eneo hilo wamefurahi kutengenezewa  barabara  ila changamoto wanayokutana nayo ni upitaji wa magari ya abiria hasa Haice na
pikipiki zinapita kwa   mwendo  wa kasi ambao ni hatari  kwa wananchi.

Amesema barabara hiyo yenye urefu wa mita  300, ipo  chini ya Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini (TARURA)  na  ni muunganiko wa barabara ya  mtaa wa
Rexona road, NHC Ngarenaro inayokwenda kuungana na NHC makao mapya.

Hii barabara kwetu kama wakazi  tumefurahi kutengenezewa barabara,ila changamoto zake imekuwa kama barabara kuu inayopitisha magari haswa
Haice kwa mwendo  kasi    ambayo ni hatari kwa wananchi,“alisema Kimaro.

 Pamela Lyimo ni mkazi wa eneo la Ngarenaro  ilipopita barabara hiyo amesema wanaishukuru Latra kwa kuchukua hatua hiyo kwani muda wote wao kama wazazi wamekuwa na wasiwasi juu ya watoto wao kutokana na kupita kwa daladala hizo katika maeneo yao kwani wanapita kwa kasi mno.

Yaani hata nilikuwa nikienda kazini nakuwa na wasiwasi watoto wangu watakapotoka shule itakuwaje ,maana hizo hiace zinavyopita kwenye hii barabara madereva hawajali ,wapo kwenye mwendo kasi

Hii barabara huwezi kumtuma mtoto dukani hadi ashikwe mkono kwaajili ya mwendo kasi wa hiace na bodaboda ni hatari tunakuwa na wasiwasi” Alisema Kimaro.

Kimaro ameomba kuwa na kusema Ili waweze  kuwa na amani kutumia barabara hii kuwe na ukomo wa mwendo pia ikiwezekana waweke bamsi kwaajili ya kuepusha ajali kwa wakazi wa eneo
husika.

Wanafunzi wanaosoma shule kama Maromboso,Levolosi,Mwangaza,Tetra ,Ngarebaro zote ni shule za msingi na sekondari ambapo wanafunzi wanatumia barabara hiyo wakati wakienda shule na kurudi majumbani

Aidha amesema dereva anapokamatwa kwa kupita njia isiyo rasmi faini yake ni shilingi laki moja kwa faini za Latra.

Kimaro ameomba na kusema Ili waweze  kuwa na amani kutumia barabara hiyo kuwe na ukomo wa mwendo katika barabara hiyo ,pia ikiwezekana waweke bamsi kwaajili ya kuepusha ajali kwa wakazi wa eneo
husika.

Wanafunzi wanaosoma shule kama Maromboso,Levolosi,Mwangaza,Tetra,Ngarebaro zote ni shule za msingi na sekondari wanatumia barabara hiyo wakati wakienda shule na kurudi majumbani

Aidha amesema dereva anapokamatwa kwa kupita njia isiyo rasmi faini yake ni shilingi laki moja kwa faini za Latra.