Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amewataka Makamanda wa Polisi
nchini kusimamia kampeni zilizoanza za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa
kuwalinda wagombea wa vyama vya siasa ambavyo vilitangaza kujitoa,
pamoja na kuwashughulikiwa bila huruma watu waliopanga kufanya vurugu.
Waziri
Lugola amesema ana taarifa za kutosha kuhusu baadhi ya watu waliopanga
kufanya vurugu wakati wa kampeni kwa lengo la kuvuruga uchaguzi huo,
aliwataka Makamanda hao kuwasaka kila kona, kuwakamata watu hao ambao
wana nia mbaya ya kuvuruga uchaguzi huo.

“Nawataka
mtende haki katika usimamizi wa uchaguzi huu, lakini wapo baadhi ya
watu ambao wamepanga kufanya vurugu, watu hao msicheke nao, watu hao
washughulikieni bila huruma, na badala ya kuwamwagia maji ya kuwasha,
sasa watumbukizeni ndani ya tenki la maji hayo ili waweze kuwashwa
zaidi, hatutaki vurugu, tunataka amani na utulivu ndani ya nchi yetu,”
Lugola.

Kwa
upande wa Vyama vya Siasa vilivyojitoa kushiriki uchaguzi huo, Lugola
alisema wagombea wapo ambao wamekataa agizo hilo la vyama vyao, hivyo
wameamua kushiriki uchaguzi huo wakigombea nafasi walizoziomba, hivyo
wanapaswa kulindwa kwa nguvu zote kwani ni haki yao kugombea.

“Wameweka
mpira kwapuni, lakini wachezaji wapo uwanjani bado wanataka
kucheza,bado wanaenda uwanjani kuwapiga wachezaji hao wasiweze kucheza,
bado wanataka kuwapiga waamuzi wasiweze kutoa pointi tatu muhimu kwa
timu ambayo imeendelea kucheza, hao muwashughulikie kiisawasawa,”