Maadhimisho ya siku ya gugu karoti na visumbufu vingine vya mazao yafanyika mkoani arusha

Katibu
Tawala wa Mkoa wa Arusha akizungumza na wadau mbalimbali waliojitokeza
kushiriki siku ya Gugu Karoti Mkoani Arusha ambapo mkutano huo
uiifanyika katika Ukumbi wa TPRI mkoani humo.




Dkt.Ester
Kimaro akizungumza na wadau mbalimbali kutoka Taasisi za Serikali na
zile za binafsi katika ukumbi wa TPRI mkoani Arusha.

Ramadhani
Kilewa ni Mtafiti kitengo cha kidhibiti visumbufu vya mimea kutoka
TPRI, amesema kuwa aina hiyo ya visumbufu vya wadudu na wanyama ni
tatizo katika mikoa yote nchini Tanzania

Erwin Kinsey Mkurugenzi wa ECHO Afrika ya Mashariki akizungumza katika siku ya Gugu Karoti iliyofanyika Mkoani Arusha.

Wakwanza
kulia ni Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Richard Kwitega ,akifuatiwa na
Dkt.Ester Kimario,aliyemuwakilisha mkurugenzi wa TPRI,wakifuatilia
mijadala inayoendekea katika siku ya gugu karoti


Katibu
Tawala wa mkoa wa Arusha Richard Kwitega akizingumza na waandishi wa
habari mara baada ya kuling’oa gugu hilo kwenye siku ya maadhimisho ya
siku ya gugu karoti na visumbufu vingine vya mazao mkoani Arusha

Ndelekwa
Kaaya ni mwenyekiti wa Kamati uhamasishaji wa kudhibiti gugu karoti
akiwa ameshikilia gugu hilo mara baada ya kuling’oa akiwa na vifaa vya
kujikinga kama anavyoonekana katika picha.

Katibu
Tawala Mkoa wa Arusha Richard Kwitega ,akifuatiwa na Dkt.Ester
Kimario,aliyemuwakilisha mkurugenzi wa TPRI,wakishiriki katika zoezi la
ung’oaji wa gugu karoti 





Zoezi
la kung’oa gugu karoti likiendelea kama inavyoonekana katika
picha,ambapo gugu hilo linakuwa kwa kasi katika mikoa mitano hapa nchini
ikiwemo Arusha,Kilimanjaro,Manyara,Kagera na Geita. 








Bwanashamba
kutoka Taasisi ya ECHO Charles Bonaventure akiwa ameshikilia  mmea wa
gugu karoti mara baada ya kuung’oa ,Kulia kwake ni Katibu tawala wa mkoa
wa Arusha Richard Kwitega  akifuatiwa na Ndugu Remigius Mchunguzi
kutoka Taasisi ya
 Utafiti wa Viwatilifu kwa ukanda wa Kitropiki (TPRI)




Washiriki wa siku ya gugu karoti pamoja na baadhi ya wanakamati wa
uhanasishaji wakiwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Richard Kwitega
wakishirikiana katika kuling’oa gugu hilo kama wanavyoonekana wakuwa
wamevaa vifaa vya kujikinga na madhara yatokanayo na gugu hilo.

Mmea
vamizi wa gugu karoti ukiwa tayari umeshang’olewa,ambapo baada ya
kunyauka utateketezwa kwa moto ikiwa ni njia moja wapo ya kuliangamiza
gugu hilo.

Ramadhani
Kilewa ni Mtafiti kitengo cha kidhibiti visumbufu vya mimea kutoka
TPRI, akitoa ufafanuzi wa jambo kwa mgeni rasmi mara baada ya kutembelea
maonyesho ya bidhaa katika siku ya gugu karoti mkoani Arusha.



Mgeni
rasmi akiwa katika picha ya pamoja na Kamati ya kamati inayoshughulikia
kuhamasisha na kuondoa mimea vamizi mkoa wa Arusha.

Na.Veronica Ignatus,Arusha




Serikali
mkoani Arusha imeitaka kamati inayoshughulikia kuhamasisha, na kuondoa
mimeavamizi ,kutoa elimu kwa kushirikiana na wataalamu kwa taasisi
mbalimbali za serikali, ikiwemo mifugo,Kilimo,Mazingira na wizara ya
Afya, mashuleni na maeneo mbalimbali ya jamii juu ya mimea vamizi wa
gugu karoti.




Kauli hiyo imetolewa na Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha Richard Kwitega,
kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ,kwenye siku ya
maadhimisho ya siku ya gugu karoti na visumbufu vingine vya mazao mkoani
Arusha ,iliyofanyika wilayani Arumeru ,katika Taasisi ya Utafiti wa
viwatilifu kwa ukanda wa kitropiki (TPRI) Mkoani Arusha.




Kwitega
amesema kuwa bila ushirikiano wa pamoja kati ya wataalamu, wadau wa
maendeleo ,kazi hiyo haitakuwa na maana wala mafanikio ,hivyo kila mmoja
analojukumu lakuhakikisha anafanyakazi kwa nafasi yake, ili elimu na
uelewa iwafikie jamii kwa ujumla katika mapambano hayo.




Ametoa
wito kwa Waandishi wa habari ambao ni wadau muhimu na jeshi la
mianvuli, kutumia vyema kalamu zao kuhabarisha jamii juu ya gugu hilo
vamizi ,kwa kutoa elimu kwa umma juu ya madhara na namana ya
kuliangamiza gugu hilo.

Mwenyekiti wa Kamati uhamasishaji wa kudhibiti gugu hilo, Ndelekwa Kaaya amesema kuwa 
dhumuni la  siku hiyo ni kuwahamasisha na kutoa Elimu ya uelewa kwa
 wadau wa kilimo,mifugo,mazingira,afya ya binadamu,viongozi wa
dini,viongozi wa kimila taasisi za Elimu ,makundi maalum watafiti
,wanasayansi ,wafanyabiashara viongozi wa siasa wafahamu kuhusu madhara



na udhibiti wa Gugu karoti na visumbufu vamizi katika mkoa wa Arusha, na mikoa mingine ambapo kuna visumbufu vamizi.




Amesema
katika siku hiyo mada mbalimbali zinazohusiana na ueneaji usambaaji na
mbinu,njia za kuzuia na kudhibiti visumbufu vamizi zitatolewa na
wataalam mbalimbali toka taasisi za serikali na sekta binafsi ili
kujenga uelewa kwa jamii ya watanzania.




Amesema
kuwa jitihada zilizofanywa na kamati katika harakati za kudhibiti gugu
hilo ni pamoja na kushirikiana na taasisi binafsi ,zimeweza kufanya
utambuzi wa visumbufu vamizi ,na kuainisha maeneo yalipovamia.




Ameinisha
changamoto zinayoikabili kamati hiyo katika kutekeleza majukumu yake ni
pamoja na ukosefu wa rasilimali fedha, kwaajili ya kuwezesha
uhamasishaji wa kuzuia na kudhibiti visumbufu vamizi, ikiwemo kuwafikia
wadau wengi katika maeneo yaliyovamiwa mkoani Arusha.



Aidha ukosefu wa vifaa vitendea kazi ,vifaa kinga vinavyotakiwa kutumika


katika
zoezi la ung’oaji wa visumbufu vamizi haswa katika maeneo mbalimbali
katika barabara za jiji la Arusha, ambapo ushirikiano mdogo kutoka kwa
wadau wenyewe katika maeneo yaliyovamiwa na visumbufu vamizi likiwemo
gugu karoti.





Mtafiti kitengo cha kidhibiti visumbufu vya mimea kutoka (TPRI)Ramadhani Kilewa  amesema
kuwa aina hiyo ya visumbufu vya wadudu na wanyama ni tatizo katika
mikoa yote nchini Tanzania,ambapo maeneo mengi yaliyovamiwa ni mashamba
ya mazao ,malisho ya


wanyama,Hifadhi
za taifa ya Arusha ,Ziwa manyara , Serengeti na Ngorongoro,maeneo ya
makazi ya watu ,maeneo ya kutunza na kusambaza nishati ya umeme ,mabwawa
ya maji kwaajili ya matumizi ya binadamu na
wanyama. 






Kilewa ameyataja  madhara yatokanayo na gugu hilo kuwa ni pamoja na magonjwa ya aleji ya ngozi kwa binadamu na wanyama,kifua kinachobana (pumu)kwa binadamu,umasikini  katika ngazi ya familia, kata ,wilaya na mkoa. (pumu)kwa binadamu.


Kiuchumi
gugu hilo linasababisha kupungua kwa mavuno ya mazao ya chakula na
biashara,Athari katika biashara ya utalii na wanyama kushindwa kupita
kwenye baadhi ya mimea vamizi,maziwa ya wanayama wanaofugwa kuwa na
uchungu kwasababu ya sumu iliyomo katika mimea vamizi,upungufu wa
malishio ya wanyama pamoja
madhara kwa afya ya udongo na uoto wa asili na uharibifu wa mazingira 






Aidha
asili ya gugu hilo kwamba ni Amerika ya Kusini,A.kati na A.Kaskazini
maeneo ya Mexico, hapa nchini Tanzania liliingia mwaka 2010  limetokea
nchini Ethiopia,ambapo mmea mmoja huweza kutoa mbegu 15,000
,25,000-100,000 na zinauwezo wa kuzaa kila baada ya miezi 4,mmea mmoja
unaweza kutoa miche kwa mara tatu,unauwezo wa kukaa
ardhini kwa miaka kumi.





“Zinaenea
kwa njia ya upepo,utengenezaji wa barabara,upepo binadamu wenyewe,Asia
Afrika,Visiwa ,Austaralia Afrika ya kusini,nchi zote za Afrika ya
Mashariki wa Afrika zaidi ya 13,kwa Tanzania taarifa iliyopo ni mikoa
mitano,inaathiri uoto wa asili,i
nazuia mbegu za mazao zisiote
,inasaidia uzaliaji wa wadudu,vimelea vya magonjwa kwenda kwenye mazao
mengine,inzi weupe”.Alisema Kilewa.