Mmafunzo yaendelea kutolewa kupitia programu jumuishi ya taifa ya makuzi na malezi ya awali ya mtoto (pjt – mmmam) mkoa wa shinyanga

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Wazazi Mkoani Shinyanga wamekumbushwa
kushiriki kikamilifu katika malezi bora ya watoto wao ili kuwaimarisha katika
hatua za ukuaji wa ubongo na kwamba hatua hiyo itawasaidia watoto kukua katika
utimilifu wao.

Hayo yamebainishwa na mwezeshaji kupitia
Programu jumuishi ya Taifa ya makuzi na malezi ya awali ya mtoto (PJT – MMMAM) Mkoa
wa Shinyanga ambaye ni meneja miradi kutoka shirika la ICS Bi. Sabrina Majikata
 pamoja na mambo mengine amesema ni
muhimu wazazi, Baba na Mama kushiriki katika malezi bora ya mtoto.

Amesema ipo changamoto ya baadhi ya wazazi
wa kiume (Baba) kushindwa kushiriki katika hatua mbalimbali za malezi bora ya
mtoto kushindwa kufikia utimilifu wao katika maisha ya kila siku.

“Kuna
changamoto kubwa sana katika suala la malezi hususan kwa ushiriki wa Baba
inaonekana Baba ushiriki wake bado siyo ule ambao unaoridhisha katika malezi ya
mtoto, unapozungumzia malezi wazazi wengi wanafikiri ni jukumu la mama peke
yake lakini tunasema mtoto anapolelewa, kusikia sauti za wazazi wote wawili na
kujifunza kupitia wazazi wote wawili inasaidia pia kuchochea ukuaji wa ubongo
wake”

“Lakini
wanaonekana ni watoto ambao inaonekana kwamba mwisho wa siku wanafikia
mafanikio yao kwa urahisi zaidi ukilinganisha na wale ambao wanapata malezi ya
mzazi mmoja peke yake kwahiyo wito kwa wababa ni jambo la msingi sana kushiriki
kwa pamoja katika malezi ya mtoto”.
amesema
Majikata

Kwa upande wake mratibu na mwezeshaji wa
Programu jumuishi ya Taifa ya makuzi na malezi ya awali ya mtoto (PJT – MMMAM)
Mkoa wa Shinyanga Bwana Tedson Ngwale amesema serikali kwa kushirikiana na
wadau mbalimbali imependekeza kujumuisha masuala ya watoto wenye ulemavu katika
programu zote za makuzi, malezi na maendeleo ya awali ya mtoto, kupitia na
kuboresha sherea, sela na miongozo juu ya haki za mtoto mwenye ulemavu, kujengea
uwezo kwa watoa huduma juu ya umuhimu wa malezi, makuzi na maendeleo ya awali
ya mtoto pamoja na kuhamasisha jamii juu ya umuhimu wa utambuzi na afua za
mapema kwa watoto wenye ulemavu.

Bwana Tedson Ngwale pia ni afisa maendeleo
ya jamii Mkoa wa Shinyanga amesema ni muhimu jamii kutambua kuwa baadhi ya aina
za ulemavu zinatatuliwa na utumiaji wa lishe bora ambapo ameeleza kuwa elimu
itaendelea kutolewa ili jamii iweze kukabiliana na ulemavu.

Amesema kupitia programu hiyo elimu
itatolewa kwa wazazi, walezi na watoa huduma namna ya kuwatambua watoto wenye
ulemavu na waliohatarini kupata ulemavu ikiwa ni pamoja na kuwezesha mtoto
kupata huduma za marekebisho mapema.

Aidha Ngwale amesema elimu hiyo itaendelea
kutolewa kwenye jamii katika suala la kuepuka mila na imani potofu
zinazochangia ukiukwaji wa haki za mtoto mwenye ulemavu.

Kupitia Programu jumuishi ya Taifa ya
makuzi na malezi ya awali ya mtoto (PJT – MMMAM) Mkoa wa Shinyanga mafunzo
maalum yameendelea kutolewa kwa watoa huduma wa serikali wakiwemo maafisa
ustawi wa jamii, maafisa maendeleo ya jamii, maafisa lishe, maafisa afya pamoja
na maafisa elimu.

Vile vile mafunzo hayo yanatolewa kwa
watoa huduma wa vituo vya malezi ya mchana ya watoto (wamiliki wa vituo pamoja
na waalimu wao) lakini pia mafunzo hayo yanatolewa kwa kwa shule binafsi
ambavyo vinavituo vya kuwalelea watoto wenye umri mdogo kabla hawajaaza darasa
la kwanza.

Washiriki wameshukuru kwa mafunzo hayo
huku wakiahidi kuwa mabalozi wazuri katika kufanikisha na kufikia malengo ya
utekelezaji wa Programu jumuishi ya Taifa ya makuzi na malezi ya awali ya mtoto
(PJT – MMMAM) Mkoa wa Shinyanga.

Mratibu na mwezeshaji wa Programu jumuishi ya Taifa ya makuzi na malezi ya awali ya mtoto (PJT – MMMAM) ambaye pia ni afisa maendeleo ya jamii Mkoa wa Shinyanga Bwana Tedson Ngwale akizungumza kwenye mafunzo hayo leo Alhamis Septemba 21,2023.

Mratibu na mwezeshaji wa Programu jumuishi ya Taifa ya makuzi na malezi ya awali ya mtoto (PJT – MMMAM) ambaye pia ni afisa maendeleo ya jamii Mkoa wa Shinyanga Bwana Tedson Ngwale akizungumza kwenye mafunzo hayo leo Alhamis Septemba 21,2023.

Mratibu na mwezeshaji wa Programu jumuishi ya Taifa ya makuzi na malezi ya awali ya mtoto (PJT – MMMAM) ambaye pia ni afisa maendeleo ya jamii Mkoa wa Shinyanga Bwana Tedson Ngwale akizungumza kwenye mafunzo hayo leo Alhamis Septemba 21,2023.

Mafunzo yakiendelea kupitia  Programu jumuishi ya Taifa ya makuzi na malezi
ya awali ya mtoto (PJT – MMMAM) Mkoa wa Shinyanga leo Alhamis Septemba 21,2023
katika ukumbi wa mikutano ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.