Malawi yahalalisha matumizi ya bangi

Nchini Malawi bangi itatumiwa kutengeneza dawa na vitambaa vya nguvu, mafuta yatokanayo na mimea, karatasi na bidhaa nyingine.

Malawi imekua nchi ya hivi karibuni iliyoko Kusini mwa Afrika kuhalalisha kisheria ukulima na uuzaji wa ndani na nje wa bangi.
Wanaotumia bangi kama kiburudisho wanaiona bangi kama , “Malawi Gold”,
yaani Thahabu ya Malawi kama wanavyoiita wenyewe, kuwa moja ya dawa
nzuri.
Lakini maafisa wamezuwia matumizi ya kisheria ya bangi kwa mtu binafsi.
Itatumiwa kutengeneza dawa na vitambaa vya nguvu, mafuta yatokanayo na mimea, karatasi na bidhaa nyingine.
Mauzo ya bangi yanaweza kuchukua nafasi ya biashara ya tumbaku, ambayo inategemewa sana na Malawi.
Nchi nyingine za Afrika zilizolegeza sheria juu ya ukulima wa mmea wa
bangi ni pamoja na Afrika Kusini, Zambia, Lesotho na Zimbabwe
Nchi zinazotumia bangi kwa kiasi kikubwa.
Lesotho
Matumizi ya bangi nchini Lesotho yanaruhusiwa tu kwa matumizi ya dawa ,
kwa kiasi kikubwa bangi hulimwa nchini humo. Miaka ya 2000 ilikadiriwa
kuwa asilimia 70 ya bangi nchini Afrika Kusini inatoka nchini Lesotho.Image captionMaeneo ya nyanda zaa juu ya Lesotho yana udongo wenye rutuba unaofaa kwa kilimo cha bangi
Wakulima nchini Lesotho wanalima bangi kwa ajili ya matumizi yao
nyumbani na kusafirisha nje ya mipaka, kutokana na hali ya umasikini
waliyonayo, wakulima wadogo nchini humo wanalima bangi miongoni mwa
mazao yao mengine kama vile mahindi kwa ajili ya kusafirisha nchini
Afrika Kusini.
Afrika Kusini
Nchini Afrika Kusini Mahakama ya kikatiba nchini Afrika kusini
ilihalalisha utumiaji wa bangi kwa watu wazima katika maeneo faragha
mwaka 2018.
Mahakama hiyo ilifikia uamuzi huo kwa kauli moja, kuruhusu watu wazima
kutumia bangi wakiwa majumbani na kuima kiasi kinachoweza kutosheleza
mahitaji binafsi.
Wanaharakati wanaounga mkono utumiaji wa bangi walisheherekea uamuzi huo
wa kihistoria wakisema ”sasa tuko huru”. Hata hivyo ni haramu kutumia
bangi katika maeneo ya Umma au kuiuza.Image captionMampho Thulo huvuna bangi bila kibali
Baraza la ukuzaji bangi nchini Afrika Kusini lilifurahia uhalalishwaji
wa matumizi ya bangi na kutoa wito kwa serikali kuwaondolea mashtaka
watu waliyopatikana na kileo hicho.
Ghana
Kwa mujibu wa Umoja wa mataifa, Ghana ni mtumiaji wa tatu wa bangi
duniani, asilimia 21.5 ya raia wake wenye umri wa kati ya miaka 15 mpaka
64 wanajihusisha na uvutaji wa bangi .
kulikuwa na mjadala wa kitaifa kuhusu kuhalalishwa kwa bangi, mjadala
ambao uligonga mwamba wakati wa siku ya kimataifa ya kupambana na dawa
za kulevya.
Mamlaka nchini humo zinasema kuwa bangi ni hatari zaidi kuliko kinywaji
chenye kilevi, na iwapo itahalalishwa madhara yake hayatahimilika.
pamoja na hayo Ghana inashirikiana na mataifa mengine ya Afrika
Magharibi kuhakikisha kuwa wanapambana kukomesha matumizi ya bangi na
usafirishaji katika ukanda wao.
Korea Kaskazini
Bangi hukua kwa wingi sana nchin Korea Kaskazini hata mashirika ya
kiserikali yamekuwa yakisafirisha kuuza nje ili kupata fedha za kigeni.
wachambuzi wa mambo wanasema haiko wazi kama kuna sheria inayopinga
matumizi ya bangi, nchi hiyo haitazami kama matumizi ya bangi ni kinyume
cha sheria.
Bangi imekuwa ikiuzwa kwenye maduka ya vyakula na hata maeneo mengine watu wakivuta bila kificho.
CHANZO- BBC