Mamlaka ya dawa na vifaa tiba (tmda) yakabidhi msaada wa dawa na taulo za kike gereza la segerea

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMDA, Bw. Adam Fimbo atembelea gereza la
Segerea na kutoa msaada wa caton 45 za taulo za kike, caton 10 za pampas
na dawa mbalimbali kwa ajili ya wanahitaji ambao ni wafungwa na
mahabusu wa gereza la Segerea.
Pichani ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa (TMDA), Bw. Adam Fimbo akimkabidhi
Mkuu wa Gereza la Segerea Afande George Wambura msaada wa katoni 45 za
taulo za kike, katoni 10 za Pampas na dawa mbalimbali kwa ajili ya
wanahitaji ambao ni wafungwa na mahabusu wa gereza la hilo jana jijini
Dar es salaam Kulia ni Dkt. Benard Nyaongo wa Zahanati ya Gereza la
Segerea na Kushoto ni Kaimu Mganga Mfawidhi wa zahanati hiyo Ispekta
Shukrani Rububula.
Mkuu wa Gereza la Segerea Afande George Wambura akimpongeza Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa TMDA, Bw. Adam Fimbo mara baada ya kukabidhiwa msaada
wa katoni 45 za taulo za kike, katoni 10 za Pampas na dawa mbalimbali
kwa ajili ya wanahitaji ambao ni wafungwa na mahabusu wa gereza la hilo
jijini Dar es salaam katikati ni Dkt. Benard Nyaongo wa Zahanati ya
Gereza la Segerea na Kaimu Mganga Mfawidhi wa zahanati hiyo Inspekta
Shukrani Rububula.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMDA, Bw. Adam Fimbo na Mkuu wa Gereza la
Segerea Afande George Wambura wakiwa katika picha ya pamoja mara baada
ya makabidhiano ya msaada huo Kulia ni Kaimu Mganga Mfawidhi wa zahanati
hiyo Ispekta Shukrani Rububula na kushoto ni Dkt. Benard Nyaongo wa
Zahanati ya Gereza la Segerea.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMDA, Bw. Adam Fimbo na Mkuu wa Gereza la
Segerea Afande George Wambura pamoja na Kaimu Mganga Mfawidhi wa
zahanati hiyo Ispekta Shukrani Rububula wakijadiliana jambo mara baada
ya kukabidhiana nyaraka zenye orodha ya dawa na vifaa vilivyotolewa kama
msaada kwa zahanati hiyo katikati ni Dkt. Benard Nyaongo wa Zahanati ya
Gereza la Segerea na kushoto ni Meneja Mawasiliano na Elimu kwa Umma,wa
Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA),Gaudensia Simwanza.
Mkuu wa Gereza la Segerea Afande George Wambura akitoa shukurani zake
kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMDA, Bw. Adam Fimbo mara baada ya
kukabidhiwa msaada huo kushoto ni Meneja Mawasiliano na Elimu kwa
Umma,wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA),Gaudensia Simwanza na
katikati ni Dkt. Benard Nyaongo wa Zahanati ya Gereza la Segerea.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMDA, Bw. Adam Fimbo akipokea zawadi ya mkoba
kutoka kwa Mkuu wa Gereza la Wanawake Segerea Afande Teopista Gauza
wakati alipotembelea gereza hilo na kukabidhi msaada wa dawa na vifaa
mbalimbali, Anayeshuhudia tukio hilo ni George Wambura Mkuu wa Gereza la
Segerea. 
Msaada wa vifaa mbalimbali pamoja na dawa uliokabidhiwa kwa George
Wambura Mkuu wa Gereza la Segerea na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba
(TMDA).
Mkuu wa Gereza la Segerea Afande George Wambura akitoa maelezo kwa kwa
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMDA, Bw. Adam Fimbo wakati alipotembelea
zahanati ya gereza hilo na kutoa msaada wa dawa na vifaa mbalimbali kwa
ajili ya wafungwa.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMDA, Bw. Adam Fimbo akizungumza jambo na Mkuu
wa Gereza la Segerea Afande George Wambura wakati alipotembelea zahanati
hiyo na kujionea huduma mbalimbali za kitabibu zinavyofanyika.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMDA, Bw. Adam Fimbo akiongozwa na Mkuu wa
Gereza la Segerea Afande George Wambura na Mganga Mfawidhi wa zahanati
hiyo Ispekta Shukrani Rububula wakati akitembelea na kujionea huduma
zinavyotolewa katika zahanati hiyo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMDA, Bw. Adam Fimbo akiongozwa na Mkuu wa
Gereza la Segerea Afande George Wambura wakiwasili katika zahanati hiyo.