Marais 10 washiriki mazishi ya robert mugabe


 Marais wa nchi 10 barani Afrika, pamoja na waliostaafu leo Jumamosi Septemba 14, 2019 wameshiriki mazishi ya Rais wa zamani wa Zimbabwe, Robert Mugabe.Mwili wa mwanamapinduzi huyo aliyefariki Septemba 6, 2019 nchini Singapore alipokuwa akipatiwa matibabu unaagwa leo katika uwanja wa Harare.

Marais hao ni Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta; Rais wa Zambia, Edgar Lungu; Rais wa Msumbiji, Filipe Nyusi; Rais wa Namibia, Hage Geingob; Rais wa Equatorial Guinea, Teodoro Mbasogo; Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa; Rais wa Madagascar, Andry Rajoelina; Rais wa Malawi, Peter Mutharika, Rais wa Angola, João Lourenço na Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa.
Rais wa Singapore, Halimah Jacob naye ameshiriki mazishi hayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *