Mashimba:mikakati madhubuti inahitajika kuimarisha vuwanda vya nyama nchini

 

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Mashauri akiwa kwenye ziara ya kukagua viwanda Mbalimbali vilivyopo mkoani Pwani kwenye ziara yenye lengo la kujionea utendaji kazi wa viwanda hivyo.

Kaimu Bodi ya Nyama Nchini Imani Sichalwe akizungumzia jitihada za Bodi ya Nyama kutatua changamoto ya vibali vya Nyama nje ya nchi kwa zile nchi ambazo viwanda vyetu vya Nyama vinahitaji kupeleka Nyama.

NaVero Ignatus,Pwani

Ili sekta ya mifugo iweze kubadilika na kuchangia kwa kiasi kikubwa kwenye pato la Taifa na kuondoa umaskini kwenye nchi ni lazima iwepo mikakati madhubuti ya kuimarisha viwanda vya ndani vya nyama nchini.

Hayo yamesemwa na waziri wa mifugo na uvuvi ,Mashimba Mashauri akiwa kwenye ziara ya kukagua na kujionea maendeleo ya viwanda mbalimbali vilivyopo mkoani pwani ambapo baada ya kujionea shughuli zinazofanywa na kiwanda cha kisasa cha nyama tanchoice kilichopo soga kibaha mkoani pwani,mheshimiwa waziri amepongeza uwekezaji huo mkubwa uliofanywa na kiwanda hicho.

Mashimba  Mashauri ameongeza kwa kusema kuwa  uwepo wa kiwanda hicho kutasaidia kubadilisha fikra za wafugaji wetu kuachana na ufugaji wa mazoea na kugeukia  kwenye ufugaji bora na wakisasa utakaosaidia kukidhi vigezo vinavyohitaji vya kuuza mifugo kwenye kiwanda hicho.

Awali akizungumzia changamoto kubwa inayowakabili kiwandani hapo Mkurugenzi mkuu wa kiwanda hicho Rashid  Abdul alimuomba Waziri kuangalia namna ya kuwasaidia kutatua changamoto ya vibali vya kusafirisha nyama nje ya nchi hasa katika nchi wanazohitaji kupeleka nyama jambo linalowakwamisha kufikia malengo waliyojiwekea.

Akizungumzia ziara hiyo ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi  Mashimba Mashauri kwenye kiwanda cha nyama cha Tanchoice kilichopo kijiji cha Soga mkoani Pwani kaimu msajili wa bodi ya nyama nchini Imani Sichalwe amesema bodi ya nyama  itaendelea kushirikiana na viwanda mbalimbali vya nyama nchini ili kuleta tija kwenye sekta ya nyama nchini.

Aidha Mashimba alisema kuwa kwa sasa bodi ya nyama inaendelea kuwasiliana na mabalozi wa nchi mbalimbali waliopo Tanzania,kuja kutembelea viwanda vya hapa Nchini vya nyama  jambo litakalo saidia kuongeza masoko ya nyama katika nchi mbalimbali.

Alisema kuwa kwa kuanza tayari bodi ya nyama imeshamwalika Mwenyekiti wa mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini ambaye ni balozi wa Comoro  Dkt Ahmada El Badaoui ambapo ameshatembelea viwanda mbalimbali vya nyama jijini Arusha, kwa mwaliko wa bodi ya nyama, na balozi huyo tayari ameahidi kuwaalika mabalozi wengine kuja kushuhudia uwekezaji wa viwanda mbalimbali vya nyama ,jambo litakalosaidia kufungua masoko ya nyama katika nchi mbalimbali.