Mashindano ya dr. samia cup shinyanga kuzinduliwa kesho mjini shinyanga timu 32 kushiriki.

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Mashindano ya Michezo ya ligi ya DR. SAMIA
CUP SHINYANGA yanatarajiwa kuzinduliwa kesho Jumamosi Agosti 26,2023 katika
uwanja wa zima moto (fire) Nguzonane mjini Shinyanga.

Mashindano hayo yameandaliwa na umoja wa
vijana wa chama cha mapinduzi UVCCM kwa kushirikiana na taasisi ya Bega kwa
Bega na kwamba timu 32 za mpira wa miguu zitashiriki Mchezo huo utakaofanyika
zaidi ya Mwezi mmoja katika Manispaa ya Shinyanga.

Mratibu wa mashindano ya DR. SAMIA CUP
SHINYANGA,  Jackline Isaro amesema
uzinduzi huo utakwenda sanjari na zoezi la kukabidhi vifaa vya michezo ikiwemo
mipira pamoja na jezi kwa kila timu.

Jackline Isaro  amesema hatua hiyo ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Rais
Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuimarisha michezo.

Amesema mashindano hayo yatatoa fursa na
kushirikisha timu mbalimbali zikiwemo timu za taasisi za serikali na taasisi
binafsi katika Mkoa wa Shinyanga  kama
vile  timu ya SHUWASA, timu za Bodaboda,
timu za Masoko pamoja na timu za Walimu.

Mwenyekiti wa jumuiya ya umoja wa vijana
wa chama cha mapinduzi UVCCM Wilaya ya Shinyanga mjini Bwana Jonathan
Madete  na Katibu wa UVCCM Wilaya ya
Shinyanga Naibu Katalambula  wamewaomba
wakazi wa Manispaa ya Shinyanga kujitokeza kwa wingi kushiriki kwenye
mashindano hayo ili kufikia malengo yaliyokusudiwa ikiwemo fursa za ajira.

Kwa upande wake katibu mkuu wa chama cha
mpira wa miguu Wilaya ya Shinyanga ambaye pia ni mratibu wa shirikisho la mpira
wa miguu Tanzania TFF Mkoa wa Shinyanga Bwana Magubika Seleman Amani amesema
atahakikisha sheria zote 17 za mpira wa miguu zinazingatiwa huku akiongeza kuwa
mashindano hayo ni fursa ya ajira kwa vijana watakao shiriki ambapo amesisitiza
timi zitakazo shiriki kuzingatia sheria na taratibu za mpira wa miguu
zilizowekwa na TFF.

Bwana Magubika ametaja viwanja 8
vitakavyotumika katika mashindano hayo ikiwemo uwanja wa Saba saba Kambarage
mjini Shinyanga, uwanja wa chuo cha ualimu Shinyanga (SHYCOM), uwanja wa kata
ya Old Shinyanga, uwanja wa shule ya msingi Kitangili, uwanja wa kata ya
Ibadakuli, uwanja wa Jasko kata ya Ngokolo, uwanja wa Ndala shule ya msingi
pamoja na uwanja wa Joshoni kata ya Lubaga katika Manispaa ya Shinyanga.

Mgeni rasmi katika uzinduzi wa mashindano
ya UVCCM SHY TOWN DR. SAMIA CUP 2023 anatarajiwa kuwa Mwenyekiti wa umoja wa
wanawake wa chama cha mapinduzi UWT Mhe.Mary Pius Chatanda na kwamba kauli mbiu
ya mashindano hayo ni SAMIA VIWANJANI.

 

Mratibu wa mashindano ya DR. SAMIA CUP
SHINYANGA,  Jackline Isaro, katikati akizungumza na
waandishi wa habari leo Ijumaa Agosti 25,2023.


Mwenyekiti wa jumuiya ya umoja wa vijana
wa chama cha mapinduzi UVCCM Wilaya ya Shinyanga mjini Bwana Jonathan
Madete  upande wa kushoto akizungumza na waandishi wa
habari leo Ijumaa Agosti 25,2023.

Katibu mkuu wa chama cha mpira wa miguu
Wilaya ya Shinyanga ambaye pia ni mratibu wa shirikisho la mpira wa miguu
Tanzania TFF Mkoa wa Shinyanga Bwana Magubika Seleman Amani katikati akizungumza na
waandishi wa habari leo Ijumaa Agosti 25,2023.

Viongozi mbalimbali 

Viongozi mbalimbali. 

Picha ya pamoja na viongozi mbalimbali baada
ya kuzungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa Agosti 25,2023 katika ukumbi wa
CCM Wilaya ya Shinyanga mjini.