Mbio za baiskeli washindi wapewa zawadi, shinyanga waadhimisha sikukuu ya wakulima nanenane 2023.

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga.

Kilele cha maadhimisho ya sikukuu ya wakulima Nanenane 2023 Mkoani
Shinyanga yamefanyika katika uwanja wa CCM Kambarage na kwamba  imefanyika michezo mbalimbali ya Baskeli kwa
wanaume na wanawake.

Maadhimisho hayo yameandaliwa na Mkurugenzi wa CM
Entertainment Bwana Clouds Malunde kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo
Kampuni ya SHY BEST ambapo washindi wa mbio za Baskeli wamepewa zawadi za fedha.

Kulwa Mahega ni mkazi wa kata ya Kizumbi Manispaa ya Shinyanga
amekuwa msindi wa kwanza mbio za Baskeli kundi A ambapo amepewa zawadi ya
Pikipiki mpya aina ya SANLG

Baadhi ya wakazi wa Mkoa wa Shinyanga wamesema maadhimisho hayo ni
chachu ya kuboresha shughuli za kilimo na uvuvi na kwamba wameomba yaendelea
kuadhimishwa kila Mwaka.

Kauli mbiu ya maonyesho ya wakulima nane nane kwa
Mwaka huu 2023 inasema vijana na wanawake ni msingi imara wa mifumo endelevu ya
chakula.

  

Maadhimisho ya sikukuu ya wakulima Nanenane leo Agosti 8, 2023
yakiendelea katika uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga na kwamba
yameandaliwa na Mkurugenzi wa CM Entertainment Bwana Clouds Malunde.