Mbunge balozi adadi aishukuru serikali kuwasaidia kuweka lami kwenye mji wa muheza

MBUNGE
wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu akizungumza wakati wa
halfa ya utiliaji saini  ya kati ya Halmashauri ya Muheza na Mkandarasi
wa Kampuni ya ujenzi ya SIMAC Limited kutoka Dar kwa ajili ya kuanza
ujenzi wa barabara za mita 800 kwenye mji huo kwa kiwango cha lami kulia
ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Muheza Nassib Mbaga na kushoto ni
Meneja wa Tarura wilaya hiyo 
Mhandisi Joseph Kahoza

 Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Muheza Nassib Mbaga akizungumza wakati wa halfa hiyo
kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu kulia ni
Katibu  wa CCM wilaya ya Muheza Mohamed Moyo 
 Meneja wa Tarura wilaya hiyo Mhandisi Joseph Kahoza akizungumza wakati wa halfa hiyo kulia ni Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajab
 MBUNGE wa Jimbo la Muheza
(CCM) Balozi Adadi Rajabu akimkabidhi nyaraka na michoro mkandarasi wa kampuni
ya ujenzi SIMAC LTD kutoka Dar Felix Chawe mara baada ya kusaini nae mkataba kwa
ajili ya kuanza ujenzi wa barabara za mita 800 katika mji wa Muheza
 MBUNGE
wa Jimbo la Muheza kushoto Balozi Adadi Rajabu (aliyevaa suti)
akisisitiza jambo kwa mkandarasi wa ujenzi huo mara baada ya kutembelea
eneo ambalo ujenzi huo utafanyika 
 MBUNGE
wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu kushoto akimsikiliza
Katibu wa CCM wilaya ya Muheza Mohamed Moyo kulia wakati walipotembelea
barabara ya sokoni wilayani humo 


MBUNGE wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu ameishukuru serikali
ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Magufuli kuwasaidia kuweka lami
baadhi ya barabara zilizopo kwenye mji huo. 
Huku akiwataka wananchi wilayani humo kumpa ushirikiano mkandarasi
ambaye anatekeleza ujenzi huo ili aweze kutekeleza kazi yake kwa wakati
kutokana na kwamba amepewa muda wa miezi saba. 


Balozi Adadi aliyasema hayo wakati wa halfa ya utiaji wa saini kati ya
kati ya Halmashauri ya Muheza na Mkandarasi wa Kampuni ya ujenzi ya
SIMAC Limited kutoka Dar kwa ajili ya kuanza ujenzi wa barabara za mita
800 kwenye mji huo. 


Alisema kwamba utiliaji saini huo umeonyesha namna serikali ya awamu ya
tano imedhamiria kuhakikisha inaboresha miundombinu kwenye miji
mbalimbali hapa nchini. 
Mbunge huyo alisema kwamba barabara ni kilomita ya pili ambayo itaanzia
Kilimanjaro Bar, Darajani, relini mpaka hospitali ya Teule Muheza na
baadae kufika mpaka kwenye kipande ambacho kinatumika na wananchi kwenye
maeneo ya karibu na soko la Muheza. 
“Serikali ya awamu ya tano imeweza kutusaidia kuweka lami ni jambo kubwa
na la faraja kubwa kwetu hivyo kwa sababu lami itawekwa kwenye mji wetu
hakikisheni mnapa ushirikiano na niwaombe msimpe vikwazo vya namna
yoyote ile “Alisema Balozi Adadi. 


Awali akizungumza wakati wa halfa hiyo Meneja wa Tarura wilaya ya Muheza
Mhandisi Joseph Kahoza alisema kwamba mkandarsi aliyekabidhi mkataba
huo ni wa barabara za mita 800 kwa ajili ya kuweka lami kwa mji wa
muheza. 
Alisema mkandarasi huyo ataanza kufanya kazi hiyo kuanzia barabara ya
Kilimanjaro darajani, relini mpaka teule ambao utakuwa na thamani ya
milioni 386 huku akieleza barabara nyengine ya mita 200 zinazokarabatiwa
mjini humo zitatumia zaidi ya milioni 60.. 
Naye kwa upande wake Mkandarasi wa kampuni ya ujenzi SIMAC LTD kutoka
Dar Felix Chawe ambao wamekabidhiwa barabara hiyo alisema kwamba
anajisikia furaha kupata nafasi ya ujenzi huo huku akihitaji ushirikiano
na kuhaidia kufanya kazi kwa uwezo wake wote na maelekezo yaliyopo
kwenye mkataba