MBUNGE wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu kulia akionyeshwa na Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga Donald Ngaire floormita za Bandari ya Tanga eneo la Raskazone mbazo
zinatumika kupima mafuta yanayotoka meli kweda kwenye matenki wakati wa ziara yake ya siku moja Bandarini
MBUNGE
wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu kulia akiwa na Kaimu Meneja wa
Bandari ya Tanga Donald Ngaire wakitazama meli zilizotia nanga bandarini
hapo wakati wa ziara yake
Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga Donald Ngaire katika akimuonyesha kitu
Baharini Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu wakati wa ziara
yake ya siku moja
Baharini Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu wakati wa ziara
yake ya siku moja
Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga Donald Ngaire katika akimuonyesha mitambo mbalimbali ya floormita za Bandari ya Tanga eneo la Raskazone mbazo
zinatumika kupima mafuta yanayotoka meli kweda kwenye matenki wakati wa ziara yake ya siku moja BandariniMbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu wakati wa ziara
yake ya siku mojaMbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu wakati wa ziara yake ya siku moja mara baada ya kumaliza ziara hiyo
Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga Donald Ngaire akizungumza
Mbunge
wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu kushoto akizungumza na Kaimu
Meneja wa Bandari ya Tanga Donald Ngaire wakati wa ziara yake
Containa likishushwa na Bandarini kama inavyoonekana
MBUNGE
wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu leo amefanya ziara ya kutembelea
Bandari ya Tanga na kufanya mazungumzo na uongozi wake kuona namna
inavyofanya shughuli zake huku akiwahaidi kuwa balozi wao katika
kuitangaza ili kuvutia wafanyabiashara kuitumia.
Ummy ambaye
alifika Bandarini hapo ikiwa ni ziara yake ya siku moja kuona namna
uboreshwaji wa Bandari hiyo ulivyofanywa jambo ambalo alikuwa akilipa
nguvu wakati wa kampeni zake zake huku akiridhishwa na kazi iliyofanywa
na katika uboreshaji.
Alisema lengo la kuitembelea ni kufanya
mazungumzo na uongozi wa Bandari hiyo kwa lengo la kuangalia utendaji
wao,mikakati yao na changamoto ambazo wanakabiliana nazo ili kuona namna
ya kuzifikisha kwenye mamlaka husika ili zipatiwe ufumbuzi.
Mbunge
Ummy alisema moja ya vipaumbele vyake wakati akiomba ridhaa ya
kuwatumikia wananchi wa Jimbo hilo ilikuwa ni kuhakikisha bandari hiyo
inakuwa kichocheo cha kasi ya ukuaji wa uchumi wa Jiji la Tanga.
Alisema
maboresho hayo ya Bandari ya Tanga yatawezesha kwa mwaka meli kubwa 400
kutia nanga Bandarini kutoka meli 157 na hivyo kuongeza fursa za
ajira,uchumi wa wakazi wa mji huo ikiwemo mzunguko wa kibiashara.
Mbunge
huyo alimshukuru Rais Dkt John Magufuli kwa kuwapatia fedha Bilioni 256
ambapo sasa kazi ya kuongeza kina na kufanya upanuzi wa Bandari hiyo
awamu ya pili unaendelea na utasaidia kuifanya bandari hiyo kuwa bora
zaidi ya awali.
Awali akizungumza wakati wa ziara hiyo Kaimu
Meneja wa Bandari ya Tanga Donald Ngaire alisema Bandari hiyo ipo kwenye
maboresho makubwa ya uboreshaji wa miundombinu pamoja na huduma.
Alisema
awamu ya pili ya utekelezaji wa kazi hiyo umeshaanza na utatekelezwa
kwa miezi 22 ambapo mara baada ya mradi huo kukamilika utawezesha meli
kubwa kutia nanga gatini na hivyo kuongeza kiwango cha mzigo
unaohudumiwa.