Na Elias Gamaya Shinyanga
Mgodi wa dhahabu Mwakitolyo kitalu namba 5 uliopo
halimashauri ya wilaya ya Shinyanga Mkoani Shinyanga kwa kutambua mchango wa
sekta ya elimu na na kutambua changamoto zinazowakabili wachimbaji, mama
wajawazito na watoto umenunua gari abulensi aina ya toyota haisi pamoja na
kuwajengea vyumba vitatu vya madarasa, ofisi moja na madawati 135 ili kuchochea
maendeleo kwenye kata hiyo.
Akisoma risala kwa mkuu wa wilaya ambae pia ni Mgeni
rasim Meneja wa mgodi wa mwakitolyo kitalu No:5 waziri Leonard amesema lengo la
kununua gari hilo ni kuwasaidia wachimbaji kuwawaisha hospitali pindi wanapo
pata ajari pia mama wajawazito pamoja na watoto.
Leonard amesema gharama za ujenzi wa madarasa hayo,
ofisi moja ya waalimu na dawati 135 umeghalimu TSH 68,891, 000 (milioni sitini
na nane laki nane na tisini na moja elfu) huku ununuzi wa gari ya wagonjwa ni
zaidi ya milioni 60
“kwa
takwimu za mwakatana 2022 tumepoteza ndugu zetu wawili kwa sababu ya kukosa
usafiri kwa kuwafikisha hospitali hivyo tumeamua kununua gari hili kwa ajili ya
kuwawahisha wachimbaji wenzetu hospitali pindi wanapopata shida, sambamba na
hilo gali hili pia litakua linabeba wagonjwa wote wa maeneo haya hususani mama
wajawazito na watoto ili kuwawahisha hospitali kwani ndio wenye uhitaji
mkubwa” amesema Meneja wa mgodi wa mwakitolyo
kitalu No:5 waziri Leonard
Kwa upandewake Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Bi. Johari
Mussa Samizi amepongeza jitihada zilizofanywa na wachimbaji hao ambapo
kasema”Niwashikuru sana kitalu No:5 kwa kutambua changamito hii kwani
unapogusa Afya na elimu umegusa maisha ya mtu mmoja mmoja hivyo niwapongeze
sana kwa hatua mliofikia tutaendelea kushirikiana nanyi bega kwa bega”
amesema Samizi
Kwa upande mwingine Samizi amewataka wazazi kupinga
vikali juu ya mmomonyoko wa maadili kwa watoto wetu na kuwataka kukaa makini na
watoto dhidi ya wimbi la Ushoga, ubakaji, usanganaji pamoja na ulawiti
unaoendelea na kusema
“Wazazi
tuwe makini na watoto wetu juu ya mmomonyoko wa maadili sikuhizi kunawimbi kuwa
la ulawiti ushoga ubakaji, na ninyi watoto msiwaluhusu mtu yyte akawagusa
sehemu zenu za siri akitaka kukugusa mwambie DON’T TOUCH HAPA NI KWANGU, toeni
taarifa kwa wazazi wenu,, Mwenyekiti wa kitongoji au kwa diwani ili hatua
zichukuliwe”amesema Samizi.
Kwa upande wao wachimbaji wadogo mgodi wa Mwakitolyo
No:5 wameeleza namna ambavyo walikua wanapata shida pindi wanapopata ajari
mgodini na kusema gari hilo litawasaidia kuokoa maisha yao
“Sisi kugologosha duarani ni kawaida tu
tunapokua humu mgodini, kunawatu wanagologosha na tunawatoa nje wakiwa bado hai
lakini usafiri unakosekana wa kuwapeleka hospitali sababu hospitali zipo mbali
Shinyanga mjini au Kahama hivyo wanafariki hapahapa tukiwanao ila kwa hilo gari
litawapeleka haraka ili wapate matibabu” amesema Henry
Kilola mchimbaji