Miradi ya maji bado ni kichefuchefu wilayani bunda

Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso akizungumza katika mkutano
Naibu Waziri Jumaa Aweso akikagua mradi wa maji Wilayani Bunda Mkoani Mara

ASHA SHABANI MARA.
Naibu
waziri wa maji Jumaa Aweso amemuagiza katibu mkuu wa wizara hiyo kufika
wilayani Bunda Mkoani Mara na kukagua maendeleo ya miradi ambayo
utekelezaji wake ni mbovu kiasi chammirafi hiyo kumaliza miaka zaidi ya
Saba miradi haujakamilika.

Miradi
ambayo utekelezaji wake ni wa kusuasua kutokana na wakandarasi wa
miradi hiyo kuwa Nina ya muda huku utekelezaji wak ukiwa chini ya
kiwango ni mradi wa  Kinyambwiga , Nyabheho ,nyangaranga pamoja na mradi
wa Maji mugeta.

Akizungumza
baada ya kujionea jinsi wakandarasi wa miradi hiyo wanavyo itekeleza
kiwango kisicho ridhisha naibu waziri wa maji Juma Aweso amemtaka katibu
mkuu wa wizara hiyo kufika na kuvunja mikataba yao kutokana na kusua
sua katika kazi hiyo.
Aidha
Aweso amesema kuwa miradi yote inayotekelezwa wilayani Bunda mkoani
Mara ni Kichefu chefu kutokana na kutokusimamiwa vema na watendaji wa
serikali ambao wapo wanaina madudu ya wakandarasi lakini wamekuwa
wakiedelea kuwapa mikataba mingine .
Awali
wananchi katika kijiji cha Kinyambwiga wakizungumzia juu ya mwenendo wa
mkandarasi wa mradi wao ameshindwa kazi kwani  miradi huo ulikuwa wa
muda mfupi lakini wanshanga kuona umemaliza miaka sita sasa bila
kukamilika.
Miradi
ya maji ya Kinyambwiga na Nyabheho inagharimu zaidi ya shilling
Billioni kumi na million mia tisa ili kujengwa chujio na usambazaji wa
maji  huku mradi wa maji wa nyangaranga na mgeta umegarimu zaidi ya
milioni 9.15 kwa ajili ya kuwapatia  wananchi wilayani humo maji.