Aaron Mrikaria, Songwe,
Watendaji wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge
Tanzania (MKURABITA) wametakiwa kuratibu taasisi za fedha zenye utayari wa kuwapatia mikopo wanufaika wa Mpango huo wenye
hatimiliki za kimila ili waweze kuanzisha shughuli mbalimbali za kiuchumi zitakazowawezesha
kuinua kipato na kuboresha maisha yao.

Agizo hilo limetolewa jana na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) wakati wa ziara
yake ya kikazi mkoani Songwe ya kukagua utekelezaji wa Miradi ya Mpango wa
Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA).

Mhe. Dkt. Mwanjelwa alitoa agizo hilo kufuatia malalamiko ya wanufaika wa
Mpango huo katika Kijiji cha Naming’ongo ambao wamesema wanashindwa kutumia
hatimiliki za kimila kupata mikopo kutokana na kukosa mwongozo na utaratibu wa upatikanaji
wa mikopo kwenye taasisi za fedha, licha ya hatimiliki hizo kupunguza migogoro
ya ardhi.

“Nawapa wiki mbili mnipe majibu ya taasisi za fedha zitakazokubaliana na
Serikali kutoa mikopo kwa kutumia hatimiliki za kimila, na kuongeza kuwa elimu
kwa umma itolewe ili wananchi waliorasimishiwa mashamba na maeneo ya biashara
wajue taratibu za kupata mikopo kwenye taasisi za fedha zilizo tayari kutoa
mikopo hiyo,” Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesisitiza.

Mhe. Dkt. Mwanjelwa amewahimiza Watendaji wa MKURABITA kuharakisha zoezi la
kutoa hatimiliki za kimila kwa wananchi waliorasimishiwa ardhi, ikizingatiwa kuwa
mchakato wa zoezi hilo huishia wilayani hivyo hakuna sababu ya ucheleweshaji.

“Kama mwananchi ameshatekeleza taratibu zote za urasimishaji, kuna haja gani
ya kusumbuliwa wakati upatikanaji wa hatimiliki za kimila ni makubaliano ambayo
yanakamilika katika ngazi ya kijiji na si wizarani,” Mhe. Dkt. Mwanjelwa amefafanua.

Aidha, Mhe. Dkt. Mwanjelwa alipata fursa ya kuona mashamba ya mpunga ya
wanufaika wa MKURABITA wa Kijiji cha Naming’ongo na kuwapongeza kwa kilimo cha
kisasa.

Jumla ya mashamba 776
yamerasimishwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Momba mkoani Songwe ambapo kati
ya hayo, hatimiliki za kimila 527 zimeshatolewa.