Mkuu wa mkoa morogoro kuwapiga jeki wahitimu mikumi veta katika ajira


Mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro
Loata Ole Sanare akipata maelezo kutoka mwanafunzi wa ngazi ya tatu
katika ya uunganishaji Stanford Ngozo namna walivyotengeneza kabati
wakati mkuu wa mkuu huyo alipotembelea karakana hiyo, mahafali ya 22 ya
Chuo cha VETA Mikumi Mkoani Morogoro.

Sehemu ya wahitimu wa chuo cha VETA Mikumi wakifurahi wakati wakiingia katika viwanja vya Mahafali katika Chuo hicho




Picha ya pamoja na wahitimu waliopata tuzo mbalimbaliKaimu
Mkuu wa Chuo cha VETA Mikumi Emmanuel Munuo akizungumza kuhusiana na
historia ya chuo  hicho na mafanikio waliyoyapata katika kuandaa vijana
wenye ujuzi .



Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Adam
Mgoi akizungumza kuhusiana na faida ya Chuo hicho kwa wakazi wa Kilosa
kupata stadi za ufundi wakati wa Mahafali ya Chuo cha VETA  Mikumi
wilayani Kilosa mkoani Morogoro.




Na Chalila Kibuda,Morogoro


Mkuu wa Mkoa wa
Morogoro Loata Ole Sanare ameahidi kuwa Balozi wakusaidia wahitimu wa
Chuo cha VETA Mikumi kwa wale wataokafanya vizuri kwenye masomo yao
baaada yakumaliza mitihani yao kwa mwaka huu


Kauli hiyo
Ameitoa wakati wa mahafali ya 22 ya chuo cha ufundi stadi mikumi mkoani
morogoro nakueleza kuwa mkoa wa morogoro unayo miradi mikubwa
inayotekelezwa kama ule mradi wa kufua umeme wa bwawa la mwl nyerere
ambao unahitaji watalaamu wanaozalishwa kutoka vyuo vya ndani na hivyo
yeye akiwa kiongozi atahakikisha watakaofaulu vizuri wanapata ajira
kwenye miradi hiyo


Mkuu huyo wa mkoa
ameeleza kuwa serikali ya awamu ya tano imedhamiria kwa dhati
kuwaendeleza vijana kwakutoa wataalumu ambao wanatoka kwenye vyuo
mbalimbali ikiwemo Veta na hivyo kila mwanafunzi anayesoma veta
anatakiwa kufahamu kuwa ipo miradi inayowahitaji wao kuitumikia ikiwemo
kujiajiri mwenyewe pamoja na kupenda kazi,kutafyta fursa,kuwa
wajasiliamali, na kujiendeleza kitaaluma ili kumudu mabadiliko ya
sayansi na teknolojia.


Nae kaimu mkuu wa
chuo Veta Mikumu Emmanuel Munuo ameziomba asasi zisizo za serikali na
wadau kuifaga mfano wa shirika la plan international kwa kutafyta vijana
walioko vijijini kutambua mahitaji yao na kasha kuwapatia mafunzo  ya
ufundi stadi na elimy ya ujasiliamali ili kuwatengenezea fursa za
kujiajiri au kuajiriwa katika sekta rasmi na isiyo rasmi.


Nao baadhi ya
wazazi na walezi wamewataka vijana wanaohitimu masomo kuwa waadilifu
nakuutumia ujuzi waliupata kwa manufaa kwa jamii na taifa pamoja
nakusoma kwa bidiii ili kuitumia fursa yakauli ya mkuu wa mkoa yakutumia
miradi iliyopo Morogoro kwakupata ajira


Jumla ya wahitimu 240,Wavulana 176 na Wasichana 64 wanahitimu kwa fani mbalimbali chuoni hapo.