Na Mapuli Misalaba, Shinyanga
Mkuu
wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi amesema ili kutokomeza vitendo vya ukatili
ni vyema jamii kuwa na maadili mema na kuishi maisha yanayompendeza Mungu.
Ameyasema hayo kwenye kikao cha pamoja na
viongozi wa kampeni ya kupinga ukatili SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga pamoja na
mambo mengine suala la utandawazi jamii imekumbushwa kuwa na mipaka katika
matumizi ya simu.
DC Samizi amesema mmomonyoko wa maadili
katika jamii ni moja ya chanzo cha ukatili hivyo ameitaka jamii kutoa
ushirikiano katika kupambana na baadhi ya watu wanaokwenda kinyume na sheria, kanuni
na taratibu zilizopo.
Mkuu
wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi amewapongeza viongozi wa
SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga kwa juhudi wanazozifanya katika kuibua na kupambana
na ukatili unaoendelea kufanyika kwenye jamii.
Kaimu afisa ustawi wa jamii Mkoa wa
Shinyanga Prisla Mushi amewasisitiza viongozi wa SMAUJATA kuendelea kuibua ukatili
unaofichwa ikiwemo ubakaji, mimba na ndoa za utotoni huku akiiomba jamii kutoa
ushirikiano.
Baadhi ya viongozi wa SMAUJATA Mkoa wa
Shinyanga akiwemo katibu wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga Bwana Daniel Kapaya
pamoja na Mwenyekiti idara ya maadili SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga Bwana Solomon
Nalinga Najulwa (Cheupe) wamesema kampeni hiyo itaendelea kuibua na kupambana
na ukatili katika jamii.
Aidha viongozi hao wamesema mwanzoni mwa
Mwezi ujao Disemba Mwaka huu 2023 katibu wa kampeni hiyo kanda ya ziwa
anatarajia kufanya ziara Mkoani Shinyanga hivyo wamesema ziara hiyo
itawanufaisha wananchi wa Mkoa wa Shinyanga na kwamba watatembelea maeneo
mbalimbali kutoa elimu ya ukatili.
Mbele ni Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari
Samizi akiwa na viongozi wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga pamoja na kaimu afisa
ustawi wa jamii Mkoa wa Shinyanga katika kikao cha pamoja ofisini kwake leo
Jumatatu Novemba 27,2023.Mbele ni Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari
Samizi akiwa na viongozi wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga pamoja na kaimu afisa
ustawi wa jamii Mkoa wa Shinyanga katika kikao cha pamoja ofisini kwake leo
Jumatatu Novemba 27,2023.
afisa ustawi wa jamii Mkoa wa Shinyanga wakimwonesha cheti ya pongeza mkuu wa
Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi.
afisa ustawi wa jamii Mkoa wa Shinyanga wakimwonesha cheti ya pongeza mkuu wa
Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi.
Kaimu afisa ustawi wa jamii Mkoa wa
Shinyanga Prisla Mushi akimwonesha cheti cha pongeza cha SMAAUJATA Mkoa wa
Shinyanga, mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi.
Mwenyekiti wa SMAUJATA Manispaa ya
Shinyanga Stella Gershom upande wa kulia akimwonesha cheti cha pongeza cha SMAAUJATA Mkoa wa
Shinyanga, mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi.
Mwenyekiti wa SMAUJATA idara ya michezo
Mkoa wa Shinyanga ambaye pia ni Polisi wa kata ya Ndala Alkwin Willa upande wa kulia akimwonesha
cheti cha pongeza cha SMAAUJATA Mkoa wa Shinyanga, mkuu wa Wilaya ya Shinyanga
Mhe. Johari Samizi.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari
Samizi akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga
pamoja na kaimu afisa ustawi wa jamii
Mkoa wa Shinyanga Prisla Mushi baada ya kikao leo Jumatatu Novemba 27,2023.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari
Samizi akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga
pamoja na kaimu afisa ustawi wa jamii
Mkoa wa Shinyanga Prisla Mushi baada ya kikao leo Jumatatu Novemba 27,2023.