Mpango wa taifa wa kupambana na uchafuzi wa mazingira ya bahari umekuja wakati muafaka-rc shigella

 

MKUU
wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza wakati akifungua warsha
ya pili ya wadau wa Mpango wa Taifa wa kujiandaa na umwagikaji wa
mafuta kwenye bahari na maziwa inayofanyika kwa wiku tatu mkoani Tanga
kushoto ni Mkurugenzi Idara ya Udhibiti uchumi Tasac Nahson Sigalla
akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Tasac
Mkurugenzi
Idara ya Udhibiti uchumi Tasac Nahson Sigalla
akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Tasac akizungumza wakati wa
warsha hiyo kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella
MKUU
wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella  akiwa ameshikilia kitabu chenye 
Mpango wa Taifa wa kujiandaa na umwagikaji wa
mafuta kwenye bahari na maziwa mara baada ya kufunga warsha ya wadau wa
mpango huo wa Taifa Jijini Tanga kushoto ni Mkurugenzi Idara ya
Udhibiti uchumi Tasac Nahson SigallaMkurugenzi
Idara ya Udhibiti uchumi Tasac Nahson Sigalla kushoto akimkabidhi Mkuu
wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kitabu chenye mpango wa wa Taifa wa
kujiandaa na umwagikaji wa
mafuta kwenye bahari na maziwaMKUU
wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella  kulia akiteta jambo na Mkurugenzi
Idara ya Udhibiti uchumi Tasac Nahson Sigalla wakati wa warsha hiyo
Wadau mbalimbali wakiwa kwenye warsha hiyo
Wadau mbalimbali wakiwa kwenye warsha hiyo
MKUU
wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella amefungua warsha ya pili ya wadau wa
Mpango wa Taifa wa kujiandaa na umwagikaji wa mafuta kwenye bahari na
maziwa inayofanyika kwa wiku tatu mkoani Tanga
 
Akizungumza wakati akifungua warsha hiyo,RC Shigella alisema Serikali kupitia Shirika la uwakala wa meli Tanzania
(Tasac) imekuja na mpango wa Taifa wa kupambana na uchafuzi wa mazingira
baharini unaotakana na umwagikaji wa mafuta kwa lengo la kuzifanya
bahari na maziwa nchini ziweze kukabiliana na umwagikaji wa mafuta
kutoka nchi jirani.
 
Alisema
mpango huo umekuja wakati muafaka kutokana na kuongezeka kwa shughuli nyingi
kwenye bahari na hivyo kupelekea uchafuzi na hatimaye kuhatarisha
matumizi ya bahari kwa watumiaji. 
Alisema
mpango huo utasaidia sana hasa wakati huu ambapo kumekuwa na matumizi
mengi ya baharini na hivyo kuna uwezekano kukatokea uchafuzi wa
mazingira. 
“Serikali
imeona ipo haja ya kuja namkakati wa mpango huu wa kujiandaa na
umwagikaji wa mafuta baharini na kwenye maziwa tumeona shughuli za
baharini zinavyozidi kuongezeka na namna ambavyo shughuli za mafuta
zinavyozidi kuwa nyingi…….., alisema RC Shigela na kuongeza kuwa
Kama
tunavyofahamu Tanzania ina maziwa mengi sana na Tanzania ina bahari ya
hindi ina zaidi ya kiliomota zaidi ya 1000 za bahari,  ni eneo kubwa
ambalo linaweza kupata uchafuzi wa baharini na uchafuzi wa baharini
unaweza ukatokana na meli zinazoleta mafuta lakini pia unaweza kutokea
sehemu ya nchi nyingine sababu sisi tupo majirani na upande wa Mombasa
na Mozambique uchafuzi unapotokea huko upo uwezekano wa kuja upande wa
kwetu wa Tanzania. 
Alisema
endapo patatokea tatizo la kumwagika mafuta nchi jirani upo uwezekano
mkubwa wa madhara yake kufika mpaka nchini mwetu na ndio maana serikali
imeona ipo haja ya kuja na mpango utakaotumika kwajili ya kukabiliana na
uchafuzi huo. 
Shigela
alisema mpango huo hauhusu eneo la baharini pekee bali unahusisha mpaka
maziwa ya Tanganyika,  Victoria na Nyasa kutokana na kuwepo kwa
muingiliano mkubwa wa shughuli za kibinadamu katika maziwa hayo. 
Hata
hivyo Shigela alisema mpango huo umekuja wakati muafaka ambapo serikali
ina dhamira ya dhati ya kuboresha mazingira ya shughuli za baharini kwa
kupanua meli zetu kwa kujenga misingi na gati nzuri ambazo zitatumia
meli kubwa lakini pia kwa kushuhudia wakati wowote ujenzi wa bomba la
mafuta kutoka Hoima nchini Uganda kuja bandari ya Tanga unaanza
kutekelezwa. 
Kwa upande
wake Mkurugenzi Idara ya Udhibiti uchumi Tasac Nahson Sigalla
akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Tasac,  alisema kuwa
majukumu ya Tasac ni kusimamia ulinzi na usalama wa usafiri majini na
kuzuia uchafuzi wa mazingira unaotokana na shughuli za usafiri wa majini
ambapo katika jukumu hilo shirika husimamia utekelezaji wa mikataba ya
kimataifa ya shirika la bahari duniani (IMO)  iliyoridhiwa na jamuhuri
ya muungano wa Tanzania. 
Mkurugenzi
huyo alisema kutokana na majukumu ya Tasac ni kazi ya msingi ya shirika
kuzuia uchafuzi wa mazingira unaotokana na umwagikaji wa mafuta kutoka
kwenye vyombo vya usafiri majini kwasababu hiyo shirika kwa kushirikiana
na taasisi nyingine za serikali liliandaa mpango wa Taifa wa kujiandaa
na umwagikaji wa mafuta kwenye bahari na maziwa mwaka 2016.
Mpango
huo ulifanyiwa mabadiliko mwaka 2020 na kuidhinishwa na waziri wa
ujenzi na uchukuzi kama nchi walibaini umuhimu wa mpango na kuuandaa
kwasababu unakidhi matakwa ya mikataba ya kimataifa ambayo Tanzania
imeridhia.