Msimamo wetu ni kusimamia yale tuliyoahidi kwa wananchi asema zelothe

 Image result for mwenyekiti wa ccm mkoa wa arusha zelothe
Na Ahmed Mahmoud,Arusha
Mwenyekiti
wa CCM Mkoa wa Arusha Zelothe Steven ameeleza msimamo wa Chama hicho
kwa wananchi ni kusimamia utekelezaji wa ilani yake walioahidi kwa
wananchi mwaka 2015 na sio vyengine.
Aliyasema
hayo kwenye ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani  kwenye ziara ya
kamati ya siasa ya CCM Mkoa na kutembelea miradi  mbalimbali ya
maendeleo katika Jiji la Arusha katika ziara hiyo alisindikizwa na
Mwenyekiti wa CCM Wilaya Joseph Massawe, wajumbe wa CCM sekretarieti ya
Mkoa, Mkuu wa Wilaya ya Arusha . Gabriel Daqarro pamoja na mkurugenzi wa
Halmashauri ya Jiji la Arusha Dkt. Maulid Madeni.
Alisema
kuwa amerishishwa Sana na utekelezaji wa miradi mbalimbali ambayo
imeelekezwa kumrahisishia mwananchi kupata huduma bora za kijamii
ikiwemo maji elimu Afya na miundombinu ya usafirishaji sanjari na
nishati ya umeme.
Zelothe
Steven alipata nafasi ya  kutembelea mradi mkubwa wa maji uliopo
 Ngaramtoni ambapo unatarajiwa kukamilika mwezi wa kumi na mbili mwaka
huu ikiwa dhumuni kubwa la mradi huo ni kuboresha hali ya upatikanaji wa
maji  kwa maana ya kuongeza mtandao wa kuwasambazia wananchi maji safi.
Akiwasilisha
taarifa za utekelezaji wa mradi huo Mkurugenzi wa AUWSA  Mhandisi Gasto
Mkawe amesema mradi huo ni sehemu ndogo tu  ya mradi mzima kwani mradi
wenyewe umegawanyika katika vipengele vitatu ili kurahisisha utekelezaji
 wake  ambapo mradi wote kwa ujumla  utagharimu shilingi billion 520 za
kitanzania pia amebainisha kuwa uzalishaji wa maji utaongezeka kwa
wastani wa lita 40,000,000 hadi lita 200,000,000 kwa siku.
Kwa
mujibu wa Mwenyekiti huyo alimpongeza Raisi wa Jamhuri ya muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuwapatia fedha hizo pia
amefurahishwa na kasi ya mkandarasi aliyepewa jukumu la kukamilisha
mradi huo kwa kasi ya utekelezaji anayofanya.
Mhe.
Zolothe Steven pia alitembelea mradi wa barabara ya Ngaramtoni
 inayoenda mpaka Usa River barabara ya (By pass) Jijini Arusha. Ujenzi
wa barabara hiyo ya lami yenye urefu wa kilomita 42.4 kutoka Ngaramtoni
hadi Usa River ambayo ikikamilika,  itapunguza msongamano wa magari
katikati ya Jiji la Arusha mradi huo utagharimu kiasi cha shilingi
bilioni 139 fedha za Kitanzania.
Sambamba
na hilo Zelothe alitembelea mradi  mwingine mkubwa wa maji Jijini
Arusha Olasiti (Burka Tenki la maji) ambao ume gharimu shilingi bilioni
2.3 akiwasilisha taarifa ya mradi huo amedokeza kuwa mradi huo utapokea
maji kiasi cha lita milioni 3 kutoka katika tenki linguine kubwa
lililopo Ngaramtoni.
Naye
Mhandisi Gasto Mkawe  alisema wanufaika wa mradi husika ni wakazi wa
Kata za Olasiti, Sombetini, Osunyai, Sokoni 1, Murieti, na Terrati
wapatao 156,320 nakuongeza kuwa pamoja na tenki hili kujengwa pia AUWSA
imepanga kujenga matenki mengine 11 katika maeneo mengine likiwemo lile
la Ngorbob, Olmoti, Mlima ccm,Themi, Moshono, Moivo na mengineyo.
Ziara
hiyo iliendelea hadi kituo cha Afya Murieti  mbapo Mhe Zolothe alipokea
taarifa ya utekelezaji  kutoka kwa Mganga Mkuu wa Jiji Dkt. Simon
Chacha.
Dkt.
Chacha alisema  kuwa mradi wa ujenzi wa kituo hicho ume gharimu jumla
ya  shilingi  bilioni moja  milioni miamoja sabini na tisa mianne
arobaini kati ya fedha hizo fedha, milioni mianne sabini na tisa mianne
arobaini zimetolewa na Halmashauri ya jiji la Arusha kwa maana ya
makusanyanyo ya ndani na Serikali kuu ilitoa  jumla ya shilingi milioni
miasaba . pia ameishukuru serekali ya Jamuhuri ya muungano chini ya Mhe.
Dkt. Joh Pombe Magufuli kwakutoa  fedha zilizo saidia kukamilika kwa
mradi huo.
DktChacha
alidokeza kuwa kituo hicho kimeanza kutoa huduma za kumuona Daktari,
maabara, kulaza wagonjwa kwa mda pia huduma za VVU na UKIMWI , huduma za
mama na mtoto pamoja na upasuaji mdogo na kusema kuwa kabla ya mwezi
huu  kuisha kituo hicho kitaanza kutoa huduma za upasuaji kwa kina mama
Dkt.
Chacha alisema kuwa lengo kubwa ni kusaidia kata ya murieti yenye
Wananchi wapatao 56,000 alieleza kuwa kata hiyo ina mitaa 13 lakini kata
yote haikuwa na kituo cha afya. Baadaye Mhe. Zelothe alitembelea Shule
ya Sekondari ya Arusha Terrat, mradi wa maji machafu uliopo Terrat ambao
upo katika hatua za mwisho za ukamilishwaji wake, Hospitali ya Wilaya
ya Engutoto na kituo cha afya Moshono.
Mhe.
Zelothe Steven amefurahishwa na utekelezaji wa ujenzi wa miradi hiyo
 alisema pia ilani inayo itekelezwa  ni  ilani ya CCM inayo elekeza kuwa
kila Kata iwe na kituo cha afya na uboreshaji wa miundo mbinu kwa hali
ya juu. “Kwa hiyo  Serikali ya CCM ni dhahiri kusema kwamba inatekeleza
kile walicho ahidi kwa wananchi wake nakuwaahidi kwamba hayo ni matokeo
ya awali yapo matokeo mazuri  yanafuata” alisema Zeloth.