Aliyemtishia mwenzake kumuua kwa bastola akamatwa

Kamanda
wa Polisi Kinondoni, Mussa Taibu amesema wamemkamata Shabani Hamis Said
ambaye anadaiwa kumtishia kwa Bastola dereva wa lori Venance John
maeneo ya Mabwe Pande, saa 3 asubuhi, October 30, 2019.


Amesema
baada ya lori la mchanga  alilokuwa anaendesha Venance kukwama bila
kupata msaada wa haraka, akatokea mshtakiwa Shabani Hamis akiwa
anaendesha gari lake aina ya Subaru na kumtaka dereva huyo ampishe ili
apite na  akamjibu hawezi kumpisha kwa sababu amekwama katika mchanga.

Baadae
wananchi wakatokea na kumpa msaada wa kumkwamua na kuondoka lakini
alipofika mbele mshtakiwa alimzuia dereva huyo wa lori na kuanza
kumtupia maneno kisha wakaanza kujibizana na kufikia hatua ya mshitakiwa
kuamua kutoa Bastola na kutishia kumuua Venance.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *