Mwenyekiti wa ccm mkoa wa shinyanga mhe. mabala awatoa hofu wananchi kwenye miradi ya maendeleo manispaa ya shinyanga

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM Mkoa wa
Shinyanga Mhe. Mabala Mlolwa amesema miradi ya maendeleo inayotekelezwa
Manispaa ya Shinyanga kupitia ilani ya chama hicho atahakikisha inakamilika ili
iweze kuwanufaisha wananchi.

Amesema hayo leo Jumamosi Juni 24,2023 wakati
akizungumza na wananchi kwenye mkutano wake wa hadhara kata ya Ibinzamata
Manispaa ya Shinyanga.

Mhe. Mabala ameeleza kuwa hivi karibuni kumetokea
mabadiliko ya mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga baadhi ya wananchi wamekuwa
na hofu kwenye miradi iliyokuwa ikitekelezwa ambapo amewahakikishia kuwa miradi
hiyo ipo kwenye ilani ya CCM na kwamba itakamilika kama ilivyokusudiwa.

“Niwatoe
mashaka miradi yote iliyokuwa imeanzishwa na ambayo bado inaendelea kuna watu
wameanza kupata mashaka kwa kusema hii miradi haitaendelea niwahakikishie
miradi yote iliyoanzishwa ipo kwenye ilani ya uchaguzi ya CCM na msimamizi wa
ilani ni mwana CCM nikiwemo mimi mwenyekiti wa Mkoa miradi yote itakamilika”.
amesema
Mwenyekiti Mabala

Amesema mpango wa CCM katika Mkoa wa Shinyanga ni
kutatua changamoto zinazowakabili wananchi ambapo amewaomba wananchi kuendelea
kukiamini chama hicho ili kuendeleza msukumo wa maendeleo kupitia viongozi
mbalimbali wa serikali na chama.

Mwenyekiti huyo wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mabala
Mlolwa amesema Chama hicho kitaendelea kuzishughulikia kero zinazowakabili
wananchi ikiwezo changamoto katika sekta ya afya, elimu pamoja na miundombinu.

Ametumia nafasi hiyo kumpongeza mbunge wa jimbo la
Shinyanga ambaye pia ni naibu waziri ofisi ya waziri mkuu anayeshughulikia kazi,
ajira na vijana Mhe. Paschal Patrobas Katambi pamoja na Mstahiki meya wa
Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko kwa kuendelea kusimamia
vizuri mapato kwenye Manispaa hiyo.

Aidha Mhe. Mabala amewaomba wananchi wa Mkoa wa
Shinyanga kuendelea kuiunga mkono serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika utekelezaji wa majukumu ili kuimarisha
uchumi wa Taifa.

  Akizungumza
mstahiki meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko amesema Halmashauri
ya Manispaa ya Shinyanga imefanya mabadiliko mbalimbali hasa katika ukusanyaji
wa mapato ya serikali ambapo malengo yaliyopo ni kukusanya takriabani bilioni
sita (6) na kwamba mpaka sasa mpango huo umekamilika kwa asiliamia mia moja huku
fedha zote yatari zimeelekezwa kwenye shughuli za maendeleo.

Amewahakikishia wananchi kuwa mapato ya Manispaa ya
Shinyanga yataendelea kuzinufaisha kata zote huku akiwaomba wakazi wa Manispaa
hiyo  kuendelea kuwaunga mkono viongozi
katika utekelezaji wa shughuli za maendeleo ikiwemo hatua mbalimbali za
kuboresha miundombinu na masoko kwa lengo la kuongeza uchumi.

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Ibinzamata Mhe. Ezekiel
Sabo amewaomba wakazi wa kata hiyo kuendelea kushirikiana katika shughuli  za maendeleo ambapo amesema ataendelea
kushughulikia changamoto zinazowakabili kupitia wataalam mbalimbali.

Diwani huyo amesema yapo maboresho mbalimbali
yanaendelea kufanyika kwenye miundombinu, masoko pamoja na mazingira ambapo
amesema atahakikisha miradi yote katika kata hiyo inafikia malengo
yaliyokusudiwa.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mabala Mlolwa
ameendelea na ziara zake kutembelea kata za Manispaa ya Shinyanga akiwa
ameambatana na wataalam mbalimbali wa serikali kwa lengo la kupokea na kutatua
kero zinazowakabili wananchi.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mabala Mlolwa
akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika  kata ya Ibinzamata Manispaa ya Shinyanga leo Jumamosi Juni 24,2023.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mabala Mlolwa
akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara leo Jumamosi Juni 24,2023
kata ya Ibinzamata Manispaa ya Shinyanga.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga mjini Mhe. Anord
Makombe akizungumza kwenye mkutano wa hadhara leo Jumamosi Juni 24,2023 uliofanyika
kata ya Ibinzamata Manispaa ya Shinyanga.

Mstahiki meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias
Ramadhan Masumbuko  akizungumza kwenye
mkutano wa hadhara leo Jumamosi Juni 24,2023 uliofanyika kata ya Ibinzamata
Manispaa ya Shinyanga.


Diwani wa kata ya Ibinzamata Mhe. Ezekiel Sabo  akizungumza kwenye mkutano wa hadhara leo
Jumamosi Juni 24,2023.

Mkutano wa hadhara ulioratibiwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga ukiendelea
katika kata ya Ibinzamata Manispaa ya Shinyanga leo Jumamosi Juni 24,2023.