Nacte yaongeza muda wa udahili kwa wanaojiunga kwa cheti na diploma


Katibu Mkuu Wizara ya Elimu
Sayansi na Tekinolojia, Dkt Leonard Akwilapo, akizungumza na wanahabari
wakati kutangaza kuongeza mda wa udahili kwa wanafunzi ngazi za Cheti na
Diploma, jijini Dodoma leo.



Mkuu wa kitengo cha Udahili wa
NACTE, Twaha Twaha, akizungumza na wanahabari wakati wa kutangaza
kuongeza mda wa udahili kwa wanafunzi ngazi za Cheti na Diploma, jijini
Dodoma leo.


…………………


Na.Alex Sonna,Dodoma


Balaza la Taifa la Elimu ya
Ufundi(NACTE) liimetangaza kuongeza muda wa udahili kwa waombaji mafunzo
kwa ngazi ya Cheti na Diploma kwa kufungua dirisha dogo la udahili kwa
lengo la kuwapa nafasi wale ambao hawakupata nafasi katika udahili wa
kwanza au kukosea chaguzi wanazostahili.


Akiongea na waandishi wa habari
jijini Dodoma, Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknologia, Dkt
Leonard Akwilapo, amesema wameamua kuongeza mda wa udahili kwa sababu
wanatambua kuna idani kubwa ya waombaji hawakupata nafasi na wengine
walikosa sifa kwa kozi husika waliyoiomba.


“Wizara imeagiza balaza la taifa
la elimu ya ufundi(NACTE) kufungua dirisha dogo la udahili kuanzia
tarehe 7 mpaka tarehe 21 Septemba, 2019,  ili kujaza nafasi zilizo
kwenye vyuo na taasisi mbalimbali za mafunzo za serikali na binafsi 
katika kada mbalimbali ambazo zina nafasi ya udahili” amesema Dkt
Akwilapo.


Aidha amesema Wizara inatoa rai
kwa wahitimu wa kidato cha nne na sita,  na wale wote waliokosa sifa za
kujiunga na mafunzo mbalimbalikutumia fulsa hiyo kufanya maombi ya
udahili upya, waombaji  wametakiwa  kuwa makini ili wasije kukosa nafasi
ya kujiunga na mwaka wa masomo kwa mwaka 2019/2020.


Aidha amebainisha kuwa kwa
waombaji wa kozi ya ualimu kwa  ngazi za  cheti na Diploma udahili
ulianza tarehe 3 mwezi wa saba hadi tarehe 30 mwezi wa Nane, 2019,
waombaji walielekezwa walielekezwa kuomba kupitia tuvuti ya NACTE kwa
waombaji wa vyuo vya serikali na vyuo binafsi walielekezwa kuomba moja
kwa moja vyuo wanavyotaka.


“Lakini hadi mwisho wa tarehe ya
udahili, waomba walikuwa 7,025 waliokamilisha maombi yao, na
waliokidhivigezo walikuwa 5,252(75%) na 1,773(25%) hawakuwa na sifa
zinazotakiwa kujiunga na mafunzo ya ualimu,  wakati nafasi zilikuwa
12,859 katika vyuo 35 vinavyotoa mafunzo hayo” amesema.


Pia amebainisha jumla ya waombaji
11,028, walichaguliwa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za
mitaa(TAMISEMI) na NACTE na kupangiwa vyuo vya mafunzo ya ualimu na
majina yao yanapatikana kwenye  tuvuti ya  ya Wizara na NACTE.


Kwa upande wake Mkuu wa kitengo
cha udahili wa NACTE, Twaha Twaha, amewatahadharisha waombaji hasa wa
kitengo cha Nessing na Clinical Medicine lazima wawe na ufaulu katika
masomo  ya Physics, Chemistry na Biology lazima vizingatiwe katika
maombi.