Baraza
la Taifa la Elimu ya Ufundi linapenda kuufahamisha umma kuwa wahitimu
wa kidato cha nne na sita wenye sifa watume maombi ya kujiunga na
mafunzo ya Ualimu ngazi ya Astashahada na Stashahada kwa mwaka wa masomo
2019/2020. Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 28/11/2019 na Masomo
yanatarajia kuanza 30/11/2019.
Waombaji
wa mafunzo haya ni wale wenye ufaulu wa Daraja la Kwanza hadi la Tatu
katika mitihani ya kidato cha NNE (kwa waombaji wa Astashahada – Miaka
Miwili) na kidato cha SITA (kwa waombaji wa Stashahada-Miaka miwili).
Waombaji watatakiwa kuomba moja kwa moja vyuoni na watasajiliwa kupitia
‘Instititutional Panel’ ya vyuo husika.

Sifa
za kujiunga na programumbalimbali za Ualimu kwa Vyuo vya Ualimu ni kama
zilivyoainishwa kwenye Kitabucha Mwongozo wa Udahili
(AdmissionGuidebook) kilichopo kwenye tovuti ya Baraza la Taifa la Elimu
ya Ufundi(NACTE) ambayo ni (www.nacte.go.tz). Kutokana na upungufu
mkubwa wa walimu wa Sayansina Hisabati, Lugha na Biashara, kipaumbele
kitatolewa kwa waombaji wa Stashahada (Miaka mitatu)waliofaulu kwa alama
‘C’ katika masomo mawili ya Sayansi/Lugha/Biashara yakufundisha.

Aidha, vyuo vinaelekezwa kuzingatia utaratibu wa udahili kwa mwaka wa masomo 2019/2020.
Imetolewa na
Ofisi ya Katibu Mtendaji
Tarehe 20/11/2019