Picha : rais magufuli asajili laini ya simu…aongeza muda wa usajili hadi januari 20,2020


Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akimkabidhi kitambulisho chake cha Taifa Msajili wa laini za Simu wa
kampuni ya simu ya Airtel Michael Martin aliokwenda kusajili Laini ya
simu kwa njia ya alama ya Vidole Mjini Chato Mkoani Geita. Desemba 27,
2019,
ambapo
ameongeza muda wa usajili siku ishirini (20) kuanzia Januari 01 hadi
Januari 20, 2020 ndiyo utakuwa mwisho wa zoezi hilo. 


Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiweka
alama ya kidole gumba alipokwenda kusajili Laini yake ya simu kwa njia ya alama
ya Vidole katika  kampuni ya simu ya
Airtel Mjini Chato Mkoani Geita. Desemba 27, 2019.Kushoto ni Msajili wa laini
za Simu wa Airtel tawi la Chato Michael Martin.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Msajili wa
laini za Simu wa kampuni ya simu ya Airtel Michael Martin baada ya kusajili
Laini yake ya simu kwa njia ya alama ya Vidole Mjini Chato Mkoani Geita Desemba 27, 2019.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akionyesha simu yake
ambayo ametoka kusajili laini yake ya simu kwa njia ya alama ya Vidole na kisha
kuzungumza na Wananchi wa Mjini Chato Mkoani Geita na Watanzania wote ambapo
ameongeza muda wa usajili siku ishirini (20) kuanzia Januari 01 hadi Januari
20, 2020 ndiyo utakuwa mwisho wa zoezi hilo. 
Awali
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe
Magufuli akielekea kusajili Laini ya simu kwa njia ya alama ya Vidole
Mjini Chato Mkoani Geita Desemba 27,2019. 
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na
Wananchi wa Mjini Chato Mkoani Geita na Watanzania wote mara baada ya kusajili
laini yake ya simu kwa njia ya alama ya Vidole ambapo Mhe. Rais ameongeza muda
wa usajili siku ishirini (20) kuanzia Januari 01 hadi Januari 20, 2020 ndiyo
utakuwa mwisho wa zoezi hilo.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na
Mjasiliamali wa Chipsi  Joseph Wandwi wa
Mjini Chato Mkoani Geita mara baada ya kusajili laini yake ya simu kwa njia ya
alama ya Vidole na kuzungumza na Wananchi hao, ambapo Mhe. Rais ameongeza muda
wa usajili siku ishirini (20) kuanzia Januari 01 hadi Januari 20, 2020ndio
utakuwa mwisho wa zoezi hilo.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na
Mjasiliamali wa Chipsi
  Joseph Wandwi wa
Mjini Chato Mkoani Geita mara baada ya kusajili laini yake ya simu kwa njia ya
alama ya Vidole na kuzungumza na Wananchi hao, ambapo Mhe. Rais ameongeza muda
wa usajili siku ishirini (20) kuanzia Januari 01 hadi Januari 20, 2020 ndiyo
utakuwa mwisho wa zoezi hilo.


Picha na Ikulu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 27 Desemba, 2019 amefanya
usajili wa laini yake ya simu kwa kutumia alama za vidole na
kuwasisitiza Watanzania wote wahakikishe laini zao za simu zinasajiliwa
kwa alamu za vidole kama ilivyoelekezwa na Mamlaka ya Mawasiliano
Tanzania (TCRA).

Rais Magufuli amefanya usajili huo
Chato Mjini katika Mkoa wa Geita. Hata hivyo, Mhe. Rais Magufuli
ameongeza siku 20 kuanzia tarehe 01 Januari, 2020 hadi tarehe 20
Januari, 2020 kwa wote ambao watashindwa kusajili laini zao katika
kipindi cha kuishia tarehe 31 Desemba, 2019 kama ilivyotangazwa na TCRA
kutokana sababu mbalimbali zikiwemo kuugua na kukamilisha upataji wa
namba ama Vitambulisho vya Taifa.

Mhe. Rais Magufuli amesisitiza kuwa
baada ya muda huo hakuna kisingizio chochote kitakachokubalika na
ameagiza TCRA kuhakikisha laini ambazo hazijasajiliwa zinazimwa.

Amefafanua kuwa usajili wa laini za
simu kwa alama za vidole ni muhimu kwa usalama wa nchi ikiwemo kuepusha
vitendo vya utapeli na ujambazi vinavyofanywa na wahalifu, ambao licha
ya wengi wao kukamatwa na vyombo vya dola wameendelea kusababisha
usumbufu na upotevu mali za wananchi hususani fedha.