Picha : wake wa viongozi tanzania wakabidhi madarasa,vyoo shule ya buhangija jumuishi shinyanga

Umoja wa wake wa viongozi nchini Tanzania ‘Ladies of New Millenium Women Group’
umekabidhi madarasa manne yenye thamani ya shilingi milioni 65.8 na
matundu 10 ya vyoo yenye thamani ya shilingi milioni 21 yanayoendelea
kujengwa katika mabweni ya shule ya Msingi Buhangija Jumuishi iliyopo
katika Manispaa ya Shinyanga ambayo ni maalumu kwa watoto wenye mahitaji
maalumu wakiwemo wenye ualbino,viziwi na wasioona.

Madarasa na matundu hayo ya vyoo
yamekabidhiwa leo Jumapili Novemba 10,2019 na Mlezi wa Umoja wa wake wa
viongozi,Maria Majaliwa kwa Waziri wa Elimu,Sayansi na
Teknolojia,Profesa Joyce Ndalichako wakati wa ziara yake mkoani
Shinyanga.

Akizungumza wakati wa kukabidhi madarasa hayo na matundu ya vyoo kwa
ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalumu, Mlezi wa Umoja wa wake wa
viongozi,Maria Majaliwa amesema umoja huo amesema madarasa hayo yataleta
tija kwa wanafunzi katika kuhakikisha wanajifunza katika mazingira
bora.

“Mheshimiwa Waziri nakukabidhi majengo mawili yenye madarasa mawili
kila moja na matundu 10 ya vyoo yanayoendelea kujengwa na yapo mbioni
kukamilika kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalumu wanaoishi bweni
ikiwa ni sehemu ya kuunga juhudi zinazofanywa na Rais wa awamu ya tano
Dkt. John Pombe Magufuli katika kuhakikisha wanafunzi wanasoma katika
mazingira bora,majengo haya yamejengwa kwa ubora wa hali ya juu kwa
gharama nafuu”,
amesema Mama Majaliwa ambaye ni Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Kassim Majaliwa.
Naye Mwenyekiti wa Umoja wa Wake wa viongozi,Tunu Pinda amesema umoja
huo pia utatoa shilingi milioni 3.6 kwa ajili ya kununua madawati
yatakayowekwa kwenye vyumba hivyo vya madarasa huku akiwasisitiza
wanafunzi kusoma kwa bidii ili waweze kutimiza ndoto zao za maisha.
Wakiwa katika shule ya Msingi Buhangija Jumuishi,wake wa viongozi
waliopo madarakani na waliostaafu wametoa zawadi mbalimbali kwa
wanafunzi wenye mahitaji maalumu wakiwemo wenye
ualbino,viziwi,wasiosikia na wenye ulemavu wa ngozi,zawadi hizo ni
pamoja na vifaa vya kujifunzia,vifaa vya kufanyia usafi,mafuta ya
kupaka,kupikia,miswaki,taulo laini,dawa za meno,sukari na kadhalika
vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni nne.
Wanawake hao pia wakiongozwa na Waziri wa Elimu,Sayansi na
Teknolojia,Prof. Joyce Ndalichako wamegawa chakula na kula pamoja na
wanafunzi wa shule ya msingi Buhangija huku wakiupongeza uongozi wa
serikali ya mkoa wa Shinyanga kwa kuendelea kuwa karibu na shule hiyo
maalumu.
Akizungumza, Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce
Ndalichako aliwapongeza wake hao wa viongozi kwa kuguswa na hali iliyopo
katika shule ya Buhangija na kuamua kusaidia kujenga madarasa ili
wanafunzi wasome katika mazingira rafiki.
“Niwapongeze sana akina mama kwa kujitoa kusaidia watoto hawa,hakika
mmekuwa mfano wa kuigwa.Niushukuru uongozi wa mkoa wa Shinyanga kwa
kusimamia ujenzi huu ambapo majengo ni mazuri,yana kiwango kikubwa cha
ubora ambapo kila jengo nimeambiwa limetumia shilingi milioni 16.4 hii
ni gharama ndogo,hongereni sana”
,amesema Prof. Ndalichako.
Katika hatua nyingine ameitoa wito kwa jamii kuachana na mila potofu
kuhusu watu wenye ualbino huku akiwataka wazazi na walezi kuacha tabia
ya kuficha watoto wenye ulemavu akisisitiza kuwa watoto wote ni sawa
wanatakiwa kupewa haki yao ya elimu.
Akitoa taarifa kwa Waziri Ndalichako, Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi
Buhangija Jumuishi,Selemani Kipanya amesema shule ya msingi Buhangija
Jumuishi ina jumla ya wanafunzi 1052 kati yao wenye mahitaji maalumu ni
230 ambao wanaishi bweni (wenye ualbino 131,viziwi 74,wasioona 25).
ANGALIA PICHA MATUKIO YALIYOJIRI
Muonekano wa majengo mawili yenye madarasa mawili kila moja yaliyojengwa
na Umoja wa wake wa viongozi nchini Tanzania ‘Ladies of New Millenium
Women Group’ katika shule ya Msingi Buhangija Jumuishi iliyopo katika
Manispaa ya Shinyanga. Majengo hayo yamekabidhiwa leo Jumapili Novemba
10,2019 na uongozi wa Umoja wa wake wa viongozi kwa Waziri wa
Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako . Picha zote na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Viongozi mbalimbali wakiwa na Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia
Prof. Joyce Ndalichako (wa pili kulia) wakiwa katika shule ya Msingi
Buhangija Jumuishi wakati wa makabidhiano ya madarasa manne na matundu
ya vyoo 10 katika shule hiyo.
Mlezi wa Umoja wa wake wa viongozi,Maria Majaliwa akisoma taarifa ya
ujenzi wa madarasa manne yaliyojengwa na umoja huo katika shule ya
Msingi Buhangija Jumuishi. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa
Shinyanga,Zainab Telack akifuatiwa na Mwenyekiti wa Umoja wa wake wa
Viongozi,Tunu Pinda na Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce
Ndalichako. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Jasinta
Mboneko.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack akizungumza wakati wa
makabidhiano ya madarasa na matundu ya vyoo yaliyojengwa na Umoja wa
wake wa viongozi nchini Tanzania.

Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia
Prof. Joyce Ndalichako akikata utepe wakati akipokea madarasa manne
yaliyojengwa na Umoja wa wake wa viongozi nchini katika shule ya Msingi Buhangija Jumuishi iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga.

Ndani ya moja ya madarasa: Kulia ni Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga,Albert Msovela akimwelezea 
Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako kuhusu ujenzi wa madarasa hayo.
Waziri
wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako na viongozi
mbalimbali pamoja na wake wa viongozi wakitoka katika moja ya madarasa
yaliyojengwa na Umoja wa wake wa viongozi nchini Tanzania.

mbalimbali,wake wa viongozi na wanafunzi wa shule ya Msingi Buhangija
Jumuishiwakipiga picha ya pamoja nje ya madarasa yaliyojengwa na Umoja
wa wake wa viongozi.

Jumuishi wakipiga picha ya pamoja nje ya madarasa yaliyojengwa na Umoja
wa wake wa viongozi.

Kulia ni Afisa Elimu mkoa wa Shinyanga,Mohammed Kahundi akifurahia na
kucheza wakati viongozi wakiongozwa na Waziri wa Elimu,Sayansi na
Teknolojia wakicheza muziki wakati wa makabidhiano ya madarasa manne.
Viongozi wakicheza muziki.
Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga,Albert
Msovela akielezea kuhusu ujenzi wa matundu ya vyoo katika shule ya
msingi Buhangija Jumuishi. Vyoo hivyo vinajengwa na Umoja wa wake wa
viongozi nchini Tanzania.

Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako
akiwapongeza wake wa viongozi kujenga madarasa na vyoo katika shule ya
msingi Buhangija Jumuishi.
Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako  akiwataka wazazi na walezi kutowabagua watoto wenye ulemavu.
Viongozi mbalimbali wa serikali na Chama Cha Mapinduzi wakimsikiliza 
Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako  katika
ukumbi wa Mikutano kwenye shule ya msingi Buhangija Jumuishi.
Wanafunzi wa shule ya msingi Buhangija Jumuishi wakitoa burudani ya
wimbo mbele ya Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce
Ndalichako.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack akiwashukuru wake wa viongozi
kwa kusaidia kujenga madarasa na vyoo katika shule ya msingi Buhangija
Jumuishi.
Mwenyekiti wa Umoja wa wake wa viongozi, Tunu Pinda akizungumza katika
ukumbi wa mikutano wa shule ya msingi Buhangija Jumuishi akielezea
shughuli mbalimbali zinazofanywa na umoja huo katika kusaidia  jamii.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Jasinta Mboneko akizungumza katika ukumbi wa mikutano shule ya msingi Buhangija.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga,Mabala Mlolwa akiwapongeza wake wa
viongozi kwa kutekeleza ilani ya CCM kwa vitendo upande wa sekta ya
elimu kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa wanafunzi.
Mwalimu Mkuu shule ya msingi Buhangija Jumuishi Seleman Kipanya akitoa taarifa kuhusu shule hiyo.
Sehemu ya wake wa viongozi na madiwani wa Manispaa ya Shinyanga wakiwa ukumbini

Wanafunzi wakiwa ukumbini.
Wanafunzi wakiwa ukumbini.
Kulia ni Mwenyekiti wa Umoja wa wake wa viongozi, Tunu Pinda akikabidhi
vifaaa vya kujifunzia wanafunzi kwa Waziri wa Elimu,Sayansi na
Teknolojia Prof. Joyce Ndalichakokwa ajili ya wanafunzi wa shule ya
msingi Buhangija Jumuishi. 

 Mwenyekiti wa Umoja wa wake wa viongozi, Tunu Pinda akikabidhi vifaaa
vya kujifunzia wanafunzi kwa Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof.
Joyce Ndalichako kwa ajili ya wanafunzi wa shule ya msingi Buhangija
Jumuishi. 

 Mwenyekiti wa Umoja wa wake wa viongozi, Tunu Pinda akikabidhi sabuni
kwa Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako kwa
ajili ya wanafunzi wa shule ya msingi Buhangija Jumuishi. 

Katibu Msaidizi wa Umoja wa wake wa viongozi,Naima Malima akielezea
kuhusu Umoja wa wake wa viongozi ambao una wanachama 61 ambao ni wake wa
viongozi waliopo madarakani na viongozi waliostaafu.
Mwalimu Mkuu shule ya msingi Buhangija Jumuishi Seleman Kipanya akitoa taarifa kuhusu shule hiyo.
Sehemu ya wake wa viongozi na madiwani wa Manispaa ya Shinyanga wakiwa ukumbini
Sehemu ya wake wa viongozi na madiwani wa Manispaa ya Shinyanga wakiwa ukumbini
Wanafunzi wakiwa ukumbini.
Wanafunzi wakiwa ukumbini.
Kulia ni Mwenyekiti wa Umoja wa wake wa viongozi, Tunu Pinda akikabidhi
vifaaa vya kujifunzia wanafunzi kwa Waziri wa Elimu,Sayansi na
Teknolojia Prof. Joyce Ndalichakokwa ajili ya wanafunzi wa shule ya
msingi Buhangija Jumuishi. 

 Mwenyekiti wa Umoja wa wake wa viongozi, Tunu Pinda akikabidhi vifaaa
vya kujifunzia wanafunzi kwa Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof.
Joyce Ndalichako kwa ajili ya wanafunzi wa shule ya msingi Buhangija
Jumuishi. 

 Mwenyekiti wa Umoja wa wake wa viongozi, Tunu Pinda akikabidhi sabuni
kwa Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako kwa
ajili ya wanafunzi wa shule ya msingi Buhangija Jumuishi. 
Sehemu ya vitu mbalimbali vilivyotolewa na Umoja wa wake wa viongozi kwa

Wake wa viongozi wakigawa vifaa mbalimbali vya shule kwa wanafunzi wa shule ya msingi Buhangija Jumuishi.
Katibu Msaidizi wa Umoja wa wake wa viongozi,Naima Malima akigawa taulo
laini kwa wanafunzi wa shule ya msingi Buhangija Jumuishi.
Zoezi la kugawa vifaa vya shule likiendelea.

Wake wa viongozi wakicheza muziki na wanafunzi wa shule ya msingi Buhangija Jumuishi.
Wake wa viongozi wakicheza na wanafunzi wa shule ya msingi Buhangija Jumuishi.
Wake wa viongozi wakiongozwa na Waziri wa Elimu,Sayansi na
Teknolojia,Prof. Joyce Ndalichako ( wa pili kushoto) wakigawa chakula
kwa wanafunzi wa shule ya Msingi Buhangija Jumuishi.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack akiwapaka sabuni na kuwanawisha
wanafunzi wa shule ya msingi Buhangija Jumuishi wakati wa kula chakula
cha mchana.
Wake wa viongozi wakiendelea kugawa chakula kwa wanafunzi wa shule ya msingi Buhangija Jumuishi.
Zoezi la kugawa chakula likiendelea.
Picha ya kumbukumbu,Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko (kushoto) na wake wa viongozi nchini Tanzania.|

Picha ya kumbukumbu,Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko (kushoto) na wake wa viongozi nchini Tanzania.