Polepole: ccm imejipanga vizuri uchaguzi serikali za mitaa

Na Ahmed Mahmoud,Arusha

CHAMA
Cha Mapinduzi(CCM),kimesema kimejipanga kikamilifu katika uchaguzi
wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 24 mwaka huu na
kimewaonya wale wote ambao wamepanga kufanya vitendo vya uvunjifu wa
amani kuacha mara moja kuchochea wananchi.

Katibu
wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa,Humphrey Polepole alitoa kauli hiyo
Novemba 17 jijini Arusha alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari
katika ofisi ya CCM Mkoa wa Arusha na kueleza kuwa ushindi wa kishindo
wanaotarajia kuupata ni kutokana na wananchi kuridhishwa na utendaji wa
serikali ya awamu ya tano.

Amevitaka
vyama vyama vya upinzani kuheshimu kanuni,sheria na taratibu za
uchaguzi na kwamba wasipange au wasiwashawishi wafuasi wao kufanya
vitendo vya uvunjifu wa amani wakati wote kuanzia kipindi cha
kampeni,upigaji kura,kuhesabu matokeo pamoja na kutangazwa kwa mshindi
kwa kuwa chama hicho kimejipanga kikamilifu.

“Wananchi
wameridhishwa na utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka
2015/2020 kwani katika kipindi cha miaka mine ya uongozi wa serikali ya
awamu ya tano miradi mingi ya maendeleo inayogusa moja kwa moja maisha
ya mwananchi wa kawaida imetekelezwa kwa kiwango kikubwa sana”alisema.

Polepole
aliitaja baadhi ya miradi ambayo imetekelezwa kwa kiwango kikubwa
katika kipindi kifupi cha miaka mine kuwa ni ujenzi wa vituo vya afya na
hosipitali za Wilaya,upatikanaji wa maji safi na salama,ujenzi wa
barabara na madaraja,usambazaji wa umeme katika maeneo mengi ya mijini
na vijijini,ujenzi wa vyumba wa madarasa,nyumba za walimu pamoja na
maabara.

Alisema
kuwa mkutano huo na wanahabari ni matokeo ya kikao kazi cha kufanya
tathmini ya kimaendeleo ya miaka minne ya uongozi wa serikali ya awamu
ya tano chini ya Rais Dkt John Pombe Magufuli na kueleza kuwa Mkoa wa
Arusha ni miongoni mwa mikoa hapa nchini ambayo miradi mingi ya
kimaendeleo imetekelezwa.

Alisema
kuwa wimbi la wananchama waliotoka kwenda vyama vya upinzani mara baada
ya mzee na Waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa kuhamia huko ndio
lililopelekea chama hicho kuanza kujitathmini na kuandaa mikakati ya
ushindi ikiwemo kurudi nyumbani kwa kiongozi huyo kumekisaidia chama
hicho kuvuna wanachama wengi zaidi kwa kipindi kifupi.

Alisema
kuwa mkutano huo na wanahabari ni matokeo ya kikao kazi cha kufanya
tathmini ya kimaendeleo ya miaka minne ya uongozi wa serikali ya awamu
ya tano chini ya Rais Dkt John Pombe Magufuli na kueleza kuwa Mkoa wa
Arusha ni miongoni mwa mikoa hapa nchini ambayo miradi mingi ya
kimaendeleo imetekelezwa.

Kadhalika
katibu huyo wa Itikadi na uenezi alieleza kushangazwa kwake na baadhi
ya vyama vya upinzani ambavyo vimetangaza kujitoa katika uchaguzi wa
serikali za mitaa na kueleza kuwa baadhi ya vyama vilivyotangaza kujitoa
havikuwahi kusimamisha mgombea hata mmoja na kuhoji wanajitoa wapi.

Awali
akimkaribisha Katibu huyo wa Itikadi na uenezi Taifa,Katibu wa CCM Mkoa
wa Arusha,Mussa Matoroka alisema kuwa kuhusu uchaguzi wa serikali za
mitaa CCM Mkoa wa Arusha imejipanga kikamilifu, kimkakati na kisayansi 
kwa kuhakikisha kuwa wanashinda kwa kishido katika uchaguzi huo.

Aliwataka
wananchi wa mkoani hapa kujitokeza kwa wingi siku ya uchaguzi ili
kutimiza haki yao ya msingi kikatiba ya kuchagua katika maeneo
mbalimbali yaliyotengwa kwa ajili ya kufanyika kwa uchaguzi huo ambapo
pia amewasishi kujiepusha na vitendo vya uvunjifu wa amani kabla na
baada ya uchaguzi.

Katika
mkutano huo katibu huo wa Itikadi na uenezi taifa aliambatana na
viongozi mbalimbali wa chama hicho ngazi ya Mkoa na Wilaya ambapo kila
mmoja alipata fursa ya kuzunguza juu ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi
katika eneo lake.