Polisi arusha wafanikiwa kukamata bunduki za mbili za kivita na nyara za serikali

Nyara za serikali zilizokamatwa
na jeshi la Polisi mkoani hapa huko wilayani Ngorongoro Tarafa ya
Loliondo kwenye Kijiji cha NAAN ikiwemo nyama ya Twiga waya za kutegea
bunduki mbili simu sita mashine mbili za kuwekea alama za videlo
zinazotumia na mawakala wa makampuni ya simu Picha na Ahmed Mahmoud
Arusha.

Kamanda wa Polisi mkoani Arusha
Jonathan Shana akiwaonyesha waandishi wa Habari Meno ya Tembo
yaliokamatwa na kikosi kazi cha polisi KDU Tanapa Hifadhi ya Ngorongoro
kwenye kijiji cha NAAN Tarafa ya Loliondo mpakani mwa Tanzania na Kenya
kama zinavyoonekana pichani picha na Ahmed Mahmoud Arusha
Na Ahmed Mahmoud APC BLOG, ARUSHA
 
JESHI la polisi mkoani hapa limefanikiwa kukamata bunduki mbili
za kivita pamoja na nyara za serikali ambazo ni nyama ya twiga pamoja na
vipande viwili vya meno ya tembo sanjari na silaha za jadi yakiwemo
mapanga,sime na visu.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoani
hapa,Jonathan Shana alizitaja silaha hizo kuwa ni AK 47 yenye namba
174364 ikiwa na risasi 6 kwenye magazine na G3 yenye namba A36011858
ikiwa na risasi 9ndani ya magazine na kwamba zilikamatwa katika eneo la
Naani lililopo katika
mpaka wa Tanzania na Kenya tarafa ya Loliondo Mkoani hapa.
Alisema kukamatwa kwa silaha hizo
kunatokana na ushirikiano kati ya jeshi la polisi,Tanapa,Hifadhi ya
Ngorongoro,kikosi dhidio ya ujangili(KDU)Kanda ya kaskazini na kikosi
kazi cha taifa kinachopambana na ujangili kanda ya ziwa katika
operesheni inayorndelea huko Loliondo.
“Bunduki hizo zilipatikana baada
ya majibizano ya risasi baina ya kikosi kazi hicho kabambe na majangili
mara baada ya kuona mashambulizi yamezidi majangili hao walitelekeza
silaha hizo na kukimbilia nchi jirani,hata hivyo kikosi kikosi hicho
kilifanikiwa kumjeruhi kwa risasi jangili mmoja ambaye pia alifanikiwa
kukimbia huku akivuja damu”alisema Shana.
Kamanda huyo wa polisi aliongeza
kuwa mnamo tarehe 10 mwezi wa 11 mwaka huu katika eneo la Oleng’usa
kijiji na kata ya oloipiri ndani ya eneo la pori tengefu la Loliondo
walifanikiwa kukamata watu wawili wanaojihusisha na ujangili ambao ni
Yamhanga Mwita(19)na Chacha
Marwa(20) wakazi wa Serengeti Mkoani Mara wakiwa wameuwa Twiga.
Alisema kuwa watuhumiwa hao
walikutwa wakiwa wanaendelea kuanika nyama hizo porini kwa ajili ya
kusafirisha baada ya kuwa wamezikata vipande vipande ambapo ndio
waliokutwa na panga,sime mbili,kisu tochi pamoja na nyaya za kutegea
wanyama zikiwa katika mafungu saba.
Kuhusu meno ya tembo alisema kuwa
tarehe 10 mwezi wa 11 mwaka huu majira ya 17:40,maeneo ya mbuyuni
wilayani Arumeru waliwakamata watu watano wakiwa na meno hayo pamoja na
pikipiki mbili aina za Kinglion namba T917 BUA na Sunlag namba MC 819
ACD ambapo walitokea wilayani Simanjiro mkoani Manyara walipokuwa
wameyahifadhi na kwamba walikuja

Mkoani hapa kwa ajili ya kuyauza.
Kadhalika Kamanda Shana alisema
kuwa polisi inawashikilia Juma Yahaya(33)na Amani Mbise(32)
wanaojishughulisha na kusajili laini za simu,wakazi wa jijini hapa kwa
tuhuma za kutumia jina la Gavana wa benki kuu ya Tanzania(BOT)Profesa
Frorence Luoga katika mitandao ya kijamii na kuwatapeli watu mbalimbali
kwa kutumia jina hilo ambapo baada ya upelelezi wamekiri kosa hilo.
“Baada ya kuwapekuwa watuhumiwa tuliwakuta na simu 6,mashine mbili ya kusajili kwa alama za vidole,laini mbalimbali,vitambulisho 9 ya wateja ambao walishawasajilia laini zao za simu na kwamba tumebabaini mtuhumiwa huyu anamiliki jumba la kifahari eneo la Sombetini jijini hapa hali ambayo aiendani na kipato chake”alisema
Aliongeza kuwa pia jeshi la polisi kwa kushirikiana na Idara ya ya ustawi wa jamii jiji la Arusha imefanya operesheni ya kuwaondoa watoto wadogo wanaofanya biashara mbalimbali ikiwemo kubebeshwa mizigo kati masoko mbalimbali ya jijini hapa ambapo waliwakamata watoto 105 ambapo kati yao 46 wana umri chini ya miaka 18 na 59 wana umri wa zaidi ya miaka 18.