Prof. mussa assad aahidi kumpa ushirikiano cag mpya…..ataja kazi yake mpya atakayoifanya kwa sasa

Mdhibiti
na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali aliyemaliza muda wake, Prof.
Mussa Assad ameahidi kumpa ushiarikiano wowote atakaouhitaji CAG mpya,
Charles Kichere kwani wao wanafahamiana kwa kipindi kirefu tangu akiwa
anafundisha katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.


Ametoa
kauli hiyo leo Jumanne Novemba 5, alipokuwa akimkabidhi Kichere ofisi
ambapo amesema kuwa akihitaji kitu kutoka kwake au kutokana na ujuzi
wake binafsi atakuwa tayari kumsaidia.

“Kichere
nimefahamiana naye kwa muda mrefu sana sio mtu mgeni kwangu hivyo
ninachoahidi ni kwamba akihitaji chochote kile kutoka kwangu binafsi au
kutokana na ujuzi wangu wa miaka mitano nitampa, siku yoyote akipiga
simu nitakuwepo kwaajili yake.

“Kichwani
kwangu mimi ni mtu ambaye ninapenda nipande bamia nilisimamie liote
liingie jikoni nile kwahiyo kwasababu hiyo katika miezi miwili iliyopita
nilianza kuwekeza katika kilimo hivyo ni nachokifikiria sasa hivi nikae
shambani kwangu na kupumzika kule lakini wakinihitaji watu wa mjini
watanipigia simu nitakuja kufanya kazi zangu,” amesema Prof. Assad.

Katika
hatua nyingine, Profesa Assad  amemshauri  CAG Kichere kuwa ni vyema
akawajengea uwezo watumishi waliopo kuliko kuwafanyia mabadiliko kwa
haraka kwa sababu hatua hiyo inaweza kuharibu utendaji wa taasisi.


“Taasisi haitakiwi kufanyiwa mabadiliko ya haraka muhimu ni kuwajengea uwezo waliopo, kinyume na hapo unaweza kuharibu taswira.
“Huwa naamini changes  zinaweza kutokea ila zitokee katika namna ambayo
zimepangwa vizuri, si mwaminifu katika mfumo wa kutoa watu wote na
kuweka new team usually lazima kutakuwa na mkanganyiko and can be very
expensive kwa institutions kama hizi ambazo mtu anajifunza kwa miaka
mingi.
“Kufikia level ya DAG lazima amefanya kazi na amekaa kwenye ofisi miaka
10 hadi 15, kwa hiyo experience yake ni muhimu kuihamishia kwa mtu
mwingine, ukifanya immediate changes unaweza kupoteza ile instution
memory,” amesema Profesa Assad