Pwani yafanya mnada wa kwanza wa korosho na kuuza kilo 156,257-ndikilo


:::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::


NA MWAMVUA MWINYI,MKURANGA
 
Mkoa wa Pwani, umefanya mnada wa kwanza wa
korosho kwa mfumo wa stakabadhi ghalani na kufanikiwa kuuza korosho yote
iliyokuwa katika maghala makuu, kilo 156,257 kwa daraja la kwanza na la
pili. 
 
Aidha baadhi ya waendesha maghala wamekewa
kuacha kupokea cha juu kwa viongozi wachache wa AMCOS ambao sio
waaminifu ,wakitaka wapokee korosho zisizo na viwango ama kupewa
stakabadhi za ghala wakati hakuna korosho zilizopelekwa kwenye maghala
yao.
 
Akizindua mnada huo huko Mkuranga ,mkuu wa mkoa
wa Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo alisema, daraja la kwanza limeuzwa
kwa bei  ya sh.2,571 ambapo korosho hizo zimenunuliwa na kampuni ya
Alpha Choice.
 
Alieleza, daraja la pili limenunuliwa kwa bei  sh.2,300 na korosho hizo zimenunuliwa na kampuni ya CDJKL.
 

Hata hivyo, Ndikilo
aliwataka wakulima kukausha korosho zao ili ziwe kavu na zenye ubora na
wakati wa msimu wa kilimo kupalilia na kufufua mikorosho ya zamani ili
kujiongezea kipato.

Ndikilo hakusita
kubainisha kwamba ,licha ya juhudi zote hizo mapokezi ya hali ya korosho
kwenyw maghala hairidhishi hivyo ukusanyaji uongezeke ili kufanya mnada
wa pili na mingine yenye mafanikio kwa wakulima.
 

“Lindi imeshafika
mnada wa saba,sisi ndio tumeanza ,tusifanye mchezo katika masuala ya
uchumi ama lenye manufaa kwetu kama hili”alisisitiza .
 

Kwa upande wake mkuu
wa wilaya ya Rufiji, Juma Njwayo alisema wilaya hiyo ina korosho kilo
107,592 na ubora ni STD na UG na uhakiki unaendelea.
 

Nae mrajisi wa mkoa
wa Pwani, Angela Nalimi aliweka bayana kuwa, mkoa unapendekeza korosho
zenye ubora stahili zitaendelea kupokelewa kwenye maghala makuu.
 

Alisema korosho nyingi pia bado zipo katika maghala ya AMCOS ambapo yatasimamiwa na kuratibiwa na chama kikuu (CORECU)

Angela alieleza ,halmashauri kupitia ofisi za ushirika zitasimamia malipo ya wakulima wote waliokusanya korosho kupitia AMCOS.