Rais magufuli kafanya uteuzi wa viongozi watano…mrema yumo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli
amefanya uteuzi wa wenyeviti 5 wa bodi za taasisi za Serikali baada ya
bodi za taasisi hizo kumaliza muda wake.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi imeeleza
kuwa wenyeviti hao wameongezewa muda baada ya vipindi vyao vya awali
kumalizika;
Kwanza, Rais Magufuli amemteua Agustino Lyatonga Mrema kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Parole.
Pili, Rais Magufuli amemteua Dkt. Harun Ramadhani Kondo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania (TPC).
Uteuzi wa Mrema na Dkt. Kondo umeanza tarehe 20 Januari, 2020.
Tatu, Rais Magufuli amemteua Prof. Mayunga Habibu Hemed Nkunya kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC).
Nne, Rais Magufuli amemteua Fidelis Kashumba Mutakyamilwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya Taifa Mipango na Matumizi ya Ardhi.
Tano, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Peter Maziku Maduki kuwa
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi
(VETA).
Uteuzi wa Prof. Nkunya, Bw. Mutakyamilwa na Bw. Maduki umeanza tarehe 17 Januari, 2020.
Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amemteua Dkt. Noel Biseko Logwa kuwa
Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa. Uteuzi wa Dkt. Logwa umeanza
tarehe 17 Januari, 2020 na kabla ya uteuzi huo alikuwa Mhadhiri na Mkuu
wa Idara ya Akiolojia na Mafunzo ya Urithi (Archeology and Heritage
Studies) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Dkt. Logwa amechukua nafasi ya Prof. Audax Mabula ambaye amestaafu.