Rais magufuli kutunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa falsafa na chuo kikuu cha dodoma kesho

Chuo
Kikuu cha Dodoma (UDOM) kesho kitamtunukia Rais Dk. John Magufuli
Shahada ya Heshima ya Daktari wa Falsafa (Honorary PhD) kwa uongozi wake
hususani katika ujenzi wa uchumi wa viwanda, kuwekeza kwenye elimu,
miundombinu, kuimarisha utawala bora, na mapambano dhidi ya rushwa.


Akizungumza
leo Jumatano Novemba 20, 2019 makamu mkuu wa chuo hicho, Profesa
Faustine Bee amesema shahada hiyo itatolewa kesho katika mahafali ya 10
ya chuo hicho.

 
Profesa
Bee amesema wahitimu 6,488 watatunukiwa astashahada, shahada,
stashahada ya juu, shahada ya umahiri, na shahada ya uzamivu.