Rais magufuli: uchaguzi ujao wa tanzania utakuwa huru na wa haki

Rais  Magufuli amesema Serikali imejipanga kuhakikisha uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba, 2020 unakuwa wa amani, uhuru na haki.

Amesema utakapofika uchaguzi huo, nchi na taasisi mbalimbali zitakaribishwa Tanzania kushuhudia.


Ametoa
kauli hiyo jana Jumanne Januari 21, 2020 alipokutana na mabalozi
wanaoziwakilisha nchi zao Tanzania katika sherehe za mwaka mpya 2020 na
chakula cha jioni zilizofanyika Ikulu, Dar es Salaam.
Amebainisha kuwa uchaguzi ni jambo muhimu, Serikali imejipanga kuandaa mazingira mazuri katika uchaguzi huo.

“Oktoba
mwaka huu wa 2020 nchi yetu itafanya uchaguzi mkuu, zoezi la uchaguzi
ni muhimu kwa nchi yoyote inayofuata misingi demokrasia, Serikali
imejipanga kuhakikisha kuwa uchaguzi mkuu unafanyika katika mazingira ya
amani, uhuru na haki,” amesema Rais Magufuli.

Amesema ukikaribia uchaguzi huo nchi mbalimbali na taasisi za zitakaribishwa Tanzania kushuhudia

“Kama
ilivyo kawaida yetu wakati ukifika tutazikaribisha nchi na taasisi
mbalimbali kuja kuangalia uchaguzi wetu ili kujionea jinsi nchi yetu
inavyokomaa katika nyanja ya demokrasia,” amesema Magufuli