Mkuu
wa majeshi wa zamani wa Pakistan ambaye pia alikuwa rais wa nchi hiyo
Pervez Musharraf amehukumiwa kifo na mahakama ya kupambana na ugaidi
nchini humo baada ya kupatikana na hatia ya uhaini.

Afisa
wa sheria wa serikali ya Pakistan Salman Nadeem amevieleza vyombo vya
habari kuwa, kwa mujibu wa Ibara ya 6, Musharraf amepatikana na hatia ya
kukiuka katiba ya Pakistan.

Kesi ya uhaini dhidi ya Pervez Musharraf, iliyotokana na hatua
aliyochukua tarehe 3 Novemba, 2007 ya kutangaza hali ya hatari nchini,
ilianza kusikilizwa mwaka 2014.

Kufuatia hatua yake hiyo ya kutangaza hali ya hatari, jenerali huyo
mstaafu wa jeshi la Pakistan alisimamisha katiba na kuwaweka kizuizini
wanasiasa waandamizi na majaji.

Mgogoro huo ulichochewa na jaribio lililofanywa na Musharraf mnamo mwezi
Machi mwaka 2007 la kumwachisha kazi Jaji Mkuu wa Mahakama ya Juu
Kabisa ya Pakistan wakati huo Iftikhar Muhammad Chaudhry, uamuzi ambao
ulikuja kutenguliwa na kubatilishwa na Mahakama ya Juu Kabisa ya nchi
hiyo.

Pervez Musharraf aliingia madarakani mwaka 1999 kupitia mapinduzi ya
kijeshi na akaitawala Pakistan kwa muda wa miaka tisa kabla ya
kuondolewa uongozini wakati chama chake kiliposhindwa katika uchaguzi
mkuu.

Rais huyo wa zamani wa Pakistan ambaye ameelekea uhamishoni yeye
mwenyewe huko Dubai katika Umoja wa Falme za Kiarabu, aliwahi huko nyuma
kukana shtaka hilo la uhaini lililokuwa likimkabili.

Hii ni mara ya kwanza katika historia ya Pakistan kwa mtawala wa zamani
wa kijeshi kuhukumiwa kifo kwa kupatikana na hatia ya kufanya uhaini
mkubwa.

Wachambuzi wa siasa nchini Pakistan wanasema, hukumu hiyo imeonyesha
kuwa hakuna yeyote mwenye kinga ya kutoshtakiwa, na ni ishara pia kwamba
Pakistan inabadilika na mfumo wake wa mahakama pia umebadilika…/