Ras tanga awaonya watumishi wa umma wanaojihusisha na biashara za magendo

KATIBU
Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi akizungumza wakati wa halfa
hiyo kulia ni Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Tanga 
Specioza Owure

 
 Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Tanga Specioza
Owure wakati wa halfa hiyo kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga
Mhandisi Zena Said kulia ni Meneja wa Bandari ya Tanga Ajuaye Msese
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Said kulia akigawa sehemu ya bidhaa ambazo zilikamatwa na kutaifishwa mara baada ya wamiliki wake kushindwa kukamilisha taratibu za forodha ambazo ni sukari mifuko 278 na mafuta ya kupikia madumu 1241na hivyo kamisha wa Idara ya forodha na Ushuru wa Bidhaa ameamua kutoa kama
msaada kwa taasisi mbalimbali hususani vituo vya watoto,wazee na watu wenye mahitaji maalumu na magereza kwa mkuu wa Magereza Mkoa wa Tanga Kamisha Msaidizi wa Jeshi la Magereza Emanuel Lwenga
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Said kulia akiwa na Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Specioza Owure wakigawa vitu hivyo 
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Said kulia akiwa na Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Specioza Owure wakigawa vitu hivyo 
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Said kulia akiwa na Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Specioza Owure wakikagua vitu hivyo kabla ya kugawa kwa walengwa
 Sehemu ya bidhaa ambazo ziligawiwa ambazo ni mafuta ya kula 
 Sehemu ya sukari ambayo iligawanywa leo
KATIBU
Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Said amewaonya watumishi wa umma
mkoani humo kuacha kujihusisha na masuala ya magendo huku akiwaambia
kwamba kufanya hivyo ni kudhoofisha juhudi za serikali kukusanya mapato.
 
Mhandisi
Zena aliyasema hayo leo wakati akikabidhi msaada kwa magereza yaliyopo
mkoa wa Tanga na Taasisi mbalimbali ikiwemo vituo vya kulelea watoto,
watu wenye mahitaji maalumu na vuti vya kulea wazee ambavyo vimetolewa
na Kamisha wa Idara ya Forodha na Ushuru wa Bidhaa TRA nchini kwa
mamlaka aliyopewa chini ya kifungu cha 217(2)(a) cha sheria za forodha
ya Jumuiya ya Afrika Mashariki cha mwaka 2004.
 
Kupitia
kifungu hicho Kamisha huyo ameamua kutoa msaada ya vyakula ambavyo ni
sukari na mafuta ya kupikia kwa magereza yaliyopo mkoa wa Tanga na
Taasisi mbalimbali ikiwemo vituo vya kulelea watoto, watu wenye mahitaji
maalumu na vituo vya kulea wazee
 
Vyakula
hivyo vinatokana na mazoezi yao ya kupambana na biashara za magendo
mkoani Tanga na bidhaa hizo zilitaifishwa baada ya wenye mizigo
kutokutoa mizigo kwa wakati na wengine kuiacha kabisa.
 
Alisema
kwamba lazima watumishi hao wa umma wawe mstari wa mbele kuwafichua
watu wanaohusika na biashaza magendo badala ya kushirikiana nao katika
kuingiza bidhaa hizo kwa njia za panya ambapo wanachangia kuikosesha
serikali mapato ambayo ndio yanasaidia kuchochea ukuaji wa maendeleo kwa
wananchi.
 
“Ndugu
zangu watumishi wa umma jiepusheni na magendo na anzeni kuwafichua
wanaoingia magendo na wananchi endelee kutoa taarifa kwani
tukishirikiana kwa pamoja tunaweza kumaliza kabisa suala la biashara za
namna hiyo “Alisema Ras Mhandisi Zena.
 
Hata
hivyo Katibu tawala huyo aliipongeza mamlaka hiyo kwa kujielekeza kwa
taasis hizo kwa kuzipa ahueni kutokana na kukabiliwa na changamoto
mbalimbali huku akiwapongeza kwa kufanya kazi kwa waledi kwenye kukamata
bidhaa hizo.
 
“Bidhaa
hizo zimekatwa kwa sababu zilitakiwa kulipa kodi ya serikali
imeshindikana na kama zingekuwa zimepita kinyemela zingeipa hasara
serikali hivyo niwapongeza TRA kwa  na Kamishna wa Forodha kwa kufanya
kazi kubwa na nzuri kupambana na vitendo vya namna hiyo”Alisema
 
 Awali
akizungumza wakati wa makabidhiano ya vitu hivyo Meneja wa Mamlaka ya
Mapato mkoani Tanga (TRA) Speciaoza Owure alisema kwamba mzigo huo
ulitaifishwa mara baada ya wamiliki wake kushindwa kukamilisha taratibu
za forodha hivyo kamisha wa Idara ya Forodha kuamua kutoa msaada kwa
taasisi mbalimbali.
 
Alizitaja
taasisi hizo ni vituo vya watoto,wazee na watu wenye mahitaji maalumu
na Magereza ambao waligawiwa vyakula hivyo na Katibu Tawala wa Mkoa wa
Tanga Mhandisi Zena Saidi katika halfa iliyofanyika mjini Tanga
 
“Kwa
niaba ya Kamisha wa Forodha tunaomba uridhie kugawa vyakula hivyo
vinavyotokana na mazoezi yao ya kupambana na biashara za magendo mkoani
Tanga na bidhaa hizo zilitaifishwa baada ya wenye mizigo kutokutoa
mizigo kwa wakati na wengine kuiacha kabisa”Alisema Meneja huyo wa TRA
Mkoa wa Tanga.
 
Alizitaja
bidhaa ambazo ziligawiwa ni mifuko ya sukari 278 yenye ujazo wa kg 50
ambazo thamani yake ya kiforodha ni milioni 12.7 na kodi ya forodha
ilitakiwa kuwa milioni 12,791,391.60 na VAT milioni 4,604,900.97 .
 
Aidha
waligawa pia madumu 1241 ya mafuta ya kula yenye lita 20 kila mmoja
thamani yake ya forodha ni milioni 43, 191, 652.14 na ushuru wake ni
milioni 15,117,078.24 na VAT yake ni milioni 10,495,571.44 kwa hiyo
thamani ya vifaa vilivyogawiwa ni vyenye thamani ya bilioni milioni
55,983,043.74 zenye thamani ya ushuru wa forodha miloni 27,908,469.84 na
kodi ya ongezeko la thamani (VAT) ni  miloni 15,100,472.41.
 
Hat
hivyo alisema vifaa vyote hivyo ambazo viligawiwa vilikuwa na thamani
ya milioni 55,983,043.74 na kodi ni sh.milioni 43,008,942.25.
 
Naye
kwa upande wake Mkuu wa Magezera Mkoa wa Tanga Kamisha wa Msaidizi
Emanuel Lwenga alisema kwamba wanashukuru kwa msaada huo kutokana na wao
kuwa na wanawahitaji wengi jumla ya wafungwa 1508 wote wanahitaji
kupata chakula.
 
Alisema
hivyo wanashuruku kiasi walichowapatia ambapo sukari wamepata jumla ya
kilo 9400 na hivyo itasaidia kuwalisha wafungwa kwa kipindi cha miezi
sita mkoa wa Tanga mzima huku mafutaa kilo 17442 waliokabidhiwa
itasaidia kuwalisha wafungwa mkoa mzima kwa mwaka mzima.
 
“Lakini
pia nitoe wito kwa wakati mwengine msisite kutuma msaada kwani bado
tunauhitaji mkubwa kwani wafungwa bado wapo na wataendelea kuwepo hivyo
misaada ni muhimu sana kwao “Alisema .