Rasmi mashindano ya dr. samia cup shinyanga yaanza ngokolo sekondari yaifunga st. joseph 3 – 0

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Mashindano maalum ya DR. SAMIA CUP
SHINYANGA yameanza rasmi leo Jumapili Agosti 27,2023 ambapo timu ya Ngokolo
Sekondari imeibuka na ushindi wa magoli matatu dhidi ya timu ya Chuo cha St.
Joseph ambayo haikupata goli katika uwanja wa SHYCOM.

Mashindano hayo yameandaliwa na taasisi ya
Bega kwa Bega kwa kushirikiana na jumuiya ya vijana wa chama cha mapinduzi
UVCCM Wilaya ya Shinyanga mjini.

Akizungumza mratibu wa mashindano ya DR.
SAMIA CUP SHINYANGA,  Jackline Isaro amewapongeza
wadau mbalimbali na wananchi waliojitokeza kwenye mechi hiyo ambapo ametaja
timu zitakazocheza kwenye mchezo unaofuta.

“Niwaombe
wananchi wapenda burudani waendelee kujitokeza na kila siku tutakuwa
tunakabidhi jezi kwa timu ambazo zinafuata leo tumekabidhi jezi peya saba ili
waweze kwenda kujiandaa vizuri”.

“Mechi
ya pili itakayofuata ni timu ya Mnara wa Voda dhidi ya timu ya Wapiga debe
mchezo huo utachezwa katika uwanja wa SHYCOM, mechi ya tatu ni Ngokolo FC dhidi
ya Kadunda, mchezo namba nne utakuwa ni timu ya Mwawaza na timu ya Ndala lakini
mchezo mwingi ni timu ya mjini Shinyanga na timu ya Bushushu kwahiyo
tutaendelea kutoa ratibu”.
amesema Mratibu Jackline
Isaro

Mgeni rasmi katika mechi hiyo ni mjumbe wa
kamati ya siasa ya Halmashauri kuu ya CCM Mkoa wa Shinyanga Bwana Benard Reuben
Shigela ambaye amezipongeza timu hizo kwa kumaliza mchezo salama.

Kwa upande wake katibu mkuu wa chama cha
mpira wa miguu Wilaya ya Shinyanga ambaye pia ni mratibu wa shirikisho la mpira
wa miguu Tanzania TFF Mkoa wa Shinyanga Bwana Seleman Magubika naye
amewapongeza waandaji wa mashindano hayo, Jumuiya ya vijana wa chama cha
mapinduzi UVCCM Wilaya ya Shinyanga mjini kwa kushirikiana na Taasisi ya Bega
kwa Bega ambapo amewaomba kuendelea kuwekeza katika michezo.

 

Awali wakati wa timu ya Ngokolo sekondari
ikicheza na timu ya chuo cha ST. Joseph leo Jumapili Agosti 27,2023 katika
uwanja wa SHYCOM mjini Shinyanga.